Mradi Wa Ajira Kwa Vijana: Fursa Sawa Kwa Vijana Katika Sekta Ya Viwanda Na Ukarimu
Dar es Salaam: Tarehe 28 Aprili 2023, Forum For International Cooperation (FIC) inafanya Career fair kama moja ya shughuli muhimu za mradi wa Ajira Kwa Vijana chini ya Ajira na Ujuzi kwa Maendeleo Afrika (E4D).
Mpango huu unaungwa mkono na Ofisi ya Waziri Mkuu wa Kazi, Vijana, Ajira na Watu Wenye Ulemavu
(PMO-LYED). Inatekelezwa nchini Tanzania na GIZ na kufadhiliwa kwa pamoja na BMZ, Umoja wa Ulaya (EU), Shirika la Ushirikiano wa Maendeleo la Norway (NORAD) na Shirika la Maendeleo la Korea (KOICA).
Malengo ya mradi ni:
.Kuimarisha uwezo wa taasisi zinazotoa mafunzo ya ufundi Tanzania katika mikoa ya Dar Es Salaam, Tanga na Dodoma kupitia mafunzo ya wakufunzi, mapitio na uboreshaji wa mitaala, kuanzisha majukwaa ya kukutanisha vijana katika sekta ya ufundi na ujuzi na waajiri kutoka sekta binafsi, upatikanaji wa rasilimali, masoko na mwonekano wa taasisi ili kuvutia vijana kujiunga na vyuo vya ufundi.
- Kutoa mafunzo, huduma za ajira na uatamizi wa biashara kwa vijana 1000 wanaotoka katika kaya zisizojiweza kijamii na kiuchumi na wale ambao wamelazimika kuacha masomo kwa sababu ya kukosa kipato.
.Kuanzisha majukwaa ya kukutanisha vijana na waajiri kutoka sekta binafsi ni mojawapo ya malengo
muhimu ambayo mradi unatarajia kufikia. Ndiyo maana Forum For International Cooperation (FIC)
kupitia mradi wa Ajira Kwa Vijana, huandaa Career fair ili kuwaunganisha vijana kutoka sekta ya ujuzi na viwanda na waajiri. Kwa muda wa miezi 18, vijana wengi chini ya mradi kutoka sekta ya ufundi na ujuzi wamepokea ufadhili wa masomo na mafunzo ya stadi laini. Mradi pia umewapa fursa ya muhimu ya kukutana na kujifunza kutoka kwa waajiri moja kwa moja mahitaji ya soko la ajira.
Zaidi ya hayo tarehe 28th. April.2023 mradi wa Ajira Kwa Vijana unazindua jukwaa linalotoa ajira
mtandaoni liitwalo Ajira, Taarifa na Mafunzo (ATM) ili kuwasaidia vijana wengi zaidi katika sekta ufundi na ujuzi kupata huduma za ajira nchini Tanzania. Mbali na kutoa matangazo ya nafasi za kazi kwa waajiriwa, ATM inatoa mafunzo mbalimbali ya stadi laini ili kuwapa vijana ujuzi unaohitajika katika soko la ajira, kuwasaidia kuandaa CV na kuwakutanisha waajiri na waajiria. Pia, ATM inasaidia maafisa
uhusiano wa viwanda na ajira katika taasisi zinazotoa Elimu na Mafunzo ya Ufundi katika kuwaunganisha wanafunzi wao na kupitia Ajira, Taarifa na Mafunzo (ATM).
Mpaka sasa baadhi ya vyuo vya ufundi na ujuzi wamejiunga katika jukwaa la ATM, kama vile Masiwani,
Yombo, Chuo cha Taifa cha Utalii na VETA- Kipawa, vimeunganishwa. Vile vile waajiri kama vile COCACOLA, SILAFRICA, PEPSI, na WILMAR wamejiandikisha kwenye jukwaa ili vijana wapate nafasi za kukutana na waajiri wakubwa .