The House of Favourite Newspapers

Mradi wa Kituo Cha Biashara na Usafirishaji Ubungo Kitachochea Ukuaji wa Uchumi Kwa Nchi Yetu

CPA Makalla amesema *EAST AFRICA COMMERCIAL & LOGISTICS CENTER* ni Kituo ambacho kinakwenda kuwa kiunganishi Kati ya China na Afrika Mashariki kwani sasa kutakuwa hakuna haja ya kwenda China ila bidhaa zitapatikana hapahapa na kuchochea Ukuaji wa Maendeleo kwani Kituo hiki kitakwenda kukuza Uchumi ndani ya Afrika Mashariki hasaTanzania  hivyo tumpongeze Dkt Samia Suluhu Hassan kwakuukwamua Mradi huu Mkubwa sana ambao utaongeza Ajira kwani maduka 2000 yapo kila Mtanzania ana fursa ya kuwekeza hivyo vyovyote Vile Wenyeji tutafaidi zaidi.
Katibu wa Itikadi, Uenezi na Mafunzo Ndugu Amos Makalla amesema hayo wakati akikagua Ujenzi wa Mradi wa Kituo cha Biashara na Usafirishaji Ubungo Zamani Stendi kuu Wilaya ya Ubungo