The House of Favourite Newspapers

MRADI WA TLED KUWAFIKIA WAJASIRIAMALI KWA ASILIMIA 77 KATIKA MIKOA SITA

Afisa Mawasiliano wa Mradi wa TLED Jemima Michael (katikati), akipata maelezo kutoka kwa mmoja mjasirimali na wawanufaika wa mradi huo Anchila Petro (kulia), wakati wa maonyesho ya 43 ya Kimataifa ya Biashara ya Dar es Salaam. 
Afisa Mawasiliano wa Mradi wa TLED Jemima Michael akizungumza wakati wa maonyesho hayo.
…Jemima Michael (katikati), akiuliza jambo kwa Mjasiriamali mdogo na mnufaika wa mradi huo Mariamu Juma, (kushoto) .
…Jemima Michael (kulia), akionesha moja ya Bidhaa iliyoandaliwa na Mashine waliotoa msaada kwa Mnufaika na mjasiriamali Selena Chibando. 

 

 

 

OFISA Mawasiliano wa Mradi wa TLED ambao ni maalumu kwa ajili ya wajasiriamali wadogo na
wakati Jemima Michael amesema lengo la mradi huo ni kukabiliana na changamoto mbalimbali za
kibiashara na hasa soko.

 

Akizungmza katika Maonesho ya Biashara ya 43 ya kimataifa yanayoendelea jijini Dar es Salaam
Michael amefafua mradi huo ni wa miaka mitano chini ya ufadhili wa Global Affairs Canada (GAC)
na ulianza Aprili mwaka 2015 hadi Machi mwaka 2020.

 

"Ni mradi wenye lengo la kukabilana na changamoto za kibiashara ambazo wajasiriamali wadogo
na wakati wanakutana nazo hasa upatikanaji na ukuaji wa masoko katika sekta ya biashara ya
kilimo,"amesema.

Ameongeza nia ya TLED ni kuoa wajasiamali wanapiga hatua katika shughuli zao za kibiashara
na kiuchumi n kuboresha utoaji wa ajira kutokana na maendeleo na huduma za kifedha kwa
wajasiriamali katika mikoa sita nchini.

 

Ameitaja mikoa hiyo ambayo imefaidika mradi huo wa TLED ni Shinyanga, Mwanza, Lindi,
Mtwara, Iringa na Njombe huku malengo mahususi ni kuhakikisha mnufaikaji wa mradi huo
anapatiwa elimu na ushauri kutoka kwa timu ya washauri wakuu (wanaojitolea) na wafanyakazi
wa mradi.

Pia amesema TLED inahakikisha wanufaikaji wa mradi huo wanaunganishwa na soko la biashara
zao, upatikanaji wa teknolojia na upatikanaji wa fedha kwaajili ya kuendeshea biashara hizo.
Akifafanua zaidi malengo mengine ya mradi huo  ni kuwafikia wajasiriamali 1,760 mpaka ukomo
wa mradi huo, ambao kwa sasa mradi huo umefikia wajasiriamali 1, 361 sawa na asilimia 77 ya
walengwa.

 

Kuhusu maonesho hayo, Michael amesema wametumia fursa hiyo kuwapa fursa wajasiliamali
kujifunza kwa kuona wenzao wanafanya nini na kuzitangaza biashara zao kimataifa kupitia jukwaa
hilo la maonesho ya biashara.

 

Kwa upande wake Mjasiriamali wa kutengeneza mikoba asili kutoka mkoani Shinyanga
ameushukuru mradi wa TLED kwa kumpa fursa ya kushiriki maonesho hayo.

Comments are closed.