The House of Favourite Newspapers

Mrema: Walionizushia Kifo ni ‘Magaidi’, Wanikome

Mzee Agustino Lyatonga Mrema.

MWENYEKITI wa Bodi ya Parole nchini na Mwenyekiti wa Chama cha TLP, mwanasiasa mkongwe, Agustino Lyatonga Mrema, amekanusha taarifa za kifo ambazo zilianza kusambaa mitandaoni mapema leo Jumanne, Januari 9, 2017.

 

Akizungumza nyumbani kwake jijini Dar es Salaam na Global TV Online, Mzee Mrema amesema;

“Kwanza nataka kusema wanaonizushia kifo wanikome, washike adabu yao, ni Mungu pekee ndiye anapanga kifo, huwezi kubuni kifo cha mtu, naomba serikali iwasake. Waliofanya hivyo mimi nasema ni ‘magaidi’, hawana kazi ya kufanya.

 

“Kuzushiwa kifo kumeleta hofu kubwa sana kw familia, marafiki na jamaa zangu, hadi Rais Magufuli amepata taarifa hizi na kumwagiza msaidizi wake afuatilie ukweli wa kifo cha Mrema. Naomba sheria ya makosa ya mtandao ianze na hili la Mrema,” alisema Mrema.

 

Kuhusu afya yake Mrema amefunguka na kusema;

“Afya yangu ni njema ni kweli nilikuwa mgonjwa tangu mwaka 2015, wakati wa kampeni na wakawa wanasema msimchague Mrema ni mgonjwa ni marehemu Mtarajiwa, ila tangu Magufuli kushika urais wake aliahidi serikali itasimamia matibabu yangu, nikapelekwa India na ile kansa iliyokuwa inanisumbua imepona kabisa”, amesema Lyatonga Mrema.

Comments are closed.