Mrembo achomwa visu akilazimishwa penzi

WAKATI wapendanao duniani wakiadhimisha Sikukuu ya Valentine’s Day kesho (Alhamisi) kwa kila mmoja kuonesha mahaba niue kwa mwenza wake, hali imekuwa mbaya kwa mrembo Winnie Jackson baada ya kuchomwa visu akilazimishwa penzi na mwanaume aliyejulikana kwa jina moja la Bariki ambaye ametajwa kuwa mpenzi wake. Risasi Mchanganyiko lina kisa kamili.

 

Akizungumza kwa uchungu akiwa nyumbani kwake, Ukonga – Banana jijini Dar, Winnie ambaye ni mfanyakazi wa kampuni moja ya mabasi yafanyayo safari mikoani alisema kuwa, alikuwa na uhusiano wa kimapenzi na mwanaume huyo, lakini walikuja kuachana baada ya kugundua kuwa amezaa na mwanamke mwingine.

 

“Niliendelea kuishi maisha ya peke yangu, japokuwa Bariki alikuwa mbishi akinilazimisha mara kwa mara tuendelee kuwa wapenzi kama zamani,” anasimulia Winnie.

Anasema siku ya tukio ambayo ni Februari 8, mwaka huu alirudi Dar akitokea Arusha kwa basi kama kawaida yake, baada ya kutua kwa kuwa ilikuwa usiku wa saa 5 alikodi bodaboda impeleke hadi kituo cha daladala cha IPP-Mwenge jijini Dar.

 

“Nilipofika kituo cha IPP nikamuona kwa mbali Bariki, kwa kuwa nilikuwa sitaki hata kumuona, nikamwambia bodaboda asinishushe hivyo tukasogea kwa mbele kidogo.”

Winnie anasema kuwa, baada ya kusogea mbele ambapo kulikuwa na giza kidogo, Bariki alitokea akiwa na bodaboda nyingine na kuanza kumshambulia kwa kumchoma visu maeneo mbalimbali mwilini mwake.

“Alininichoma visu shingoni, mgongoni na kwenye masikio huku akinilazimisha nimpende.

 

“Baadaye alikimbia na kuniacha damu nyingi zikinimwagika. Wasamaria wema walitokea na kunikimbiza katika Kituo cha Polisi, Mabatini nikapatiwa PF3 kwa ajili ya kupatiwa matibabu,” alisema Winnie akionesha majeraha hayo.

Mrembo huyo alifungua kesi katika kituo hicho kwa namba KJN/RB/862/2019, KUJERUHI ambapo jeshi la polisi linamsaka Bariki kama mtuhumiwa namba moja wa tukio hilo la kinyama.

 

STORI: Andrew Carlos, Risasi Mchanganyiko

Kilichomuua GODZILLA, Dada Asimulia “Aliona Watu Wanamfata”

Toa comment