Mrembo Ajaribu Kujiua Mara Mbili Mfululizo Kisa Mapenzi

Mrembo na mwigizaji mahiri kutoka nchini Ghana mwenye shepu matata, Princess Shyngle.

MREMBO na mwigizaji mahiri kutoka nchini Ghana mwenye shepu matata, Princess Shyngle amelazwa katika hospitali moja nchini Marekani baada ya kujaribu kujiua, likiwa ni jaribio lake la pili ndani ya kipindi cha miaka mitatu.

 

Video iliyopostiwa katika akaunti ya mtandao wa kijamii wa Instagram ya mwanadada huyo, inamuonesha akiwa ndani ya gari la kubebea wagonjwa (ambulance) akikimbizwa hospitalini huku chini ya video hiyo kukiwa na maneno ‘Depression is real’ akimaanisha msongo wa mawazo siyo kitu cha kutania.

 

Inaelezwa kwamba mwanadada huyo mwenye asili ya nchini Gambia, anadaiwa kutaka kujiua kwa kumeza idadi kubwa ya vidonge ambavyo bado havijafahamika ambapo aliokolewa na wasamaria wema akiwa katika hali mbaya na kukimbizwa hospitalini.

Hii ni mara ya pili kwa mrembo huyo kujaribu kujiua, mara ya kwanza ikiwa ni mwaka 2018 ambapo alimeza idadi kubwa ya vidonge sambamba na dawa ya kuondoa madoa kwa lengo la kukatisha uhai wake akiwa nchini Nigeria.

 

Inaelezwa kwamba jirani yake ndiye aliyemuokoa na kumkimbiza katika Hospitali ya Vedic Lifecare Hospital iliyopo Lekki nchini Nigeria.


Bado chanzo cha mwigizaji huyo kutaka kujiua hakijafahamika lakini inaelezwa kwamba tukio hili limekuja siku chache baada ya Shyngle kutangaza kupeana talaka na mumewe, Gibou Bala Gaye waliyedumu naye kwa muda wa miezi mitatu kwenye ndoa yao.

Katika maelezo yake, alieleza kwamba ameamua kuachana na mumewe huyo kutokana na kuwa na kawaida ya kumfanyia vitendo vya ukatili wa kijinsia, akaambatanisha na ushahidi wa sauti ya mumewe akikiri kumfanyia vitendo hivyo vya kikatili.

 

Ndoa ya wawili hao ilifungwa Januari, mwaka huu na kabla ya mumewe huyo, alikuwa akitoka kimapenzi na staa mwingine nchini humo, Fredrick Badji ambaye uhusiano wao uliyeyuka baada ya mwanaume huyo kukamatwa Januari, 2020 na kufungwa jela zikiwa ni siku chache tangu walipoanzisha uhusiano wao.Tecno


Toa comment