Mrembo amburuza Dude polisi

dudeMrembo anayedai kuzaa na mwigizaji Kulwa Kikumba ‘Dude’, Ester Eliakim akiwa na mtoto huyo.

GLADNESS MALLYA

MREMBO anayedai kuzaa na mwigizaji Kulwa Kikumba ‘Dude’, Ester Eliakim amekwenda polisi, Kituo cha Stakishari kumshtaki mwigizaji huyo akidai hampi matumizi ya mtoto anayedai kuzaa naye.

dude
Mwigizaji Kulwa Kikumba ‘Dude’.

Licha ya Dude kumkana motto huyo, mrembo huyo amesema ana uhakika mtoto huyo amezaa na Dude lakini kinachomsikitisha kila anampomuomba matumizi, staa huyo amekuwa akimtukana badala ya kumjibu vizuri. “Nimempeleka polisi pale Stakishari. Nikapelekwa Dawati la Jinsia. Amepigiwa simu ya kuitwa akadai hayupo Dar na kuahidi akirudi atafika ili tutafute muafaka,” alisema Ester.

Alipotafutwa Dude kuhusiana na ishu hiyo, aliendelea kusisitiza kwamba hamtambui mrembo huyo bali anataka kujitafutia umaarufu kupitia jina lake.

“Nilishasema simjui huyo mtu bwana, aniache, atakuwa anatafuta umaarufu tu,” alisema Dude.


Loading...

Toa comment