The House of Favourite Newspapers

Mrembo Apigwa Kikatili Na Ex – Husband Nusu Kufa, Asimulia Kwa Uchungu… – Video

0
Mrembo aliyejitambulisha kwa jina la Doroth Msuya,

Mrembo aliyejitambulisha kwa jina la Doroth Msuya mwenye umri wa miaka 26 amedai kupigwa kikatili na mtu aliyedai ni mtalaka wake (ex-husband).
Kwa mujibu wa Doroth, mkazi wa Kimara jijini Dar es Salaam, kabla ya kutengana na mwanaume aliyemtaja kwa jina la Mfaume, walidumu kwenye ndoa yapata miaka sita na kujaaliwa watoto wawili pamoja.
Katika mahojiano maalum na Global TV, Doroth anasimulia kwa uchungu akiwa na maumivu makali yanayotokana na vidonda anaomba msaada wa kibinadamu baada ya kupitia unyanyasaji ndani ya ndoa kutoka kwa mzazi mwenzake.
Doroth anasema kuwa amejeruhiwa vibaya sehemu tofauti ikiwemo machoni kama anavyoonekana, kung’olewa kucha, kujeruhiwa maeneo mengine mwilini na kutishiwa maisha kwa jumla na mzazi mwenzake huyo.
“Inawezekana vipi mtu anayekulelea watoto wako, analipa ada ya watoto wako, kodi na bili zote unampiga kama hivi umempa mwanamke talaka lakini bado unamtoa kucha na kumuumiza kiasi hiki pamoja na madeni yote aliyoniachia, manyanyaso ya ndugu zake haya ndiyo malipo.
“Kosa langu kulalamika kuhusu matunzo, napambana na biashara zangu bado anakuja kufanya fujo kwangu na kuniibia…”

Mrembo amepigwa kikatili na mchumba wake huku watoto wake wakishuhudia ameongea na Global TV Online Kimara jijini Dar.

Leave A Reply