The House of Favourite Newspapers

MREMBO: Nimelala Apartment na Harmonize Siku 3 – Video

0

DAR: Baada ya kusambaa kwa video inayodaiwa kuonesha kuwa amefumaniwa akiwa na staa wa Bongo Fleva, Rajab Abdul ‘Harmonize’, mrembo mwenye umbo matata la kuvunja chaga Bongo; Nicole Joyberry, ameibuka na kueleza kwa upande wake kuhusu sakata hilo, Ijumaa lina full story!

 

NI WIKI HII

Mapema wiki hii, video inayodaiwa ya mpenzi wa Harmonize au Harmo, Sarah Michelotti ilivuja ikidaiwa kuwa alikuwa amekwenda kumfumania Nicole nyumbani kwake, Mbezi- Beach jijini Dar.

Akizungumza na Gazeti la IJUMAA, Nicole alifungukia mambo mengi ikiwemo suala la kulala na Harmo kwenye apartment (kota) moja kwa takriban siku tatu.

MADAI YALIVYOANZA

Awali, madai ya fumanizi hilo yalikuja baada ya Harmo kuposti picha na video za wimbo wake mpya uitwao Bedroom kwenye akaunti yake ya Instagram ikimuonesha akiwa na Nicole kitandani, jambo lililoibua maswali mengi.

Kuna ambao walidai kuwa, Harmo kwa namna yoyote atakuwa ametembea na mwanadada huyo kutokana na mvuto wake, lakini mara kadhaa yeye mwenyewe alikanusha madai hayo.

 

VIDEO SASA…

Wakati watu wakiendelea kujiuliza kulikoni huko mitandaoni kutokana na posti mbalimbali za Harmo na Nicole, ghafla ikaibuliwa video inayodaiwa kuwa ni ya fumanizi na kuanza kusambaa kama moto wa kifuu.

Kwenye video hiyo, inasikika sauti ambayo ilidaiwa kuwa ni ya mpenzi wa Harmo, Sarah akifoka baada ya kumfumania mumewe akiwa na Nicole nyumbani kwake, Mbezi-Beach jijini Dar, mapema wiki hii.

HUYU HAPA NICOLE

Ili mambo yasiwe mengi, Gazeti la IJUMAA lilimtafuta Nicole na kupiga naye stori kuhusu ishu hiyo ambapo alifunguka kwamba, hawezi kushiriki mapenzi na mwanamuziki huyo kwa sababu anamheshimu na ni mume wa mtu.

“Unajua kwanza mimi siyo video queen, lakini niliamua kushiriki kwenye Wimbo wa Harmonize kwa sababu nilitaka kumsaidia tu na ukweli ni kwamba, sijalipwa pesa yoyote, nilifanya kama msaada tu,” alisema Nicole.

AWASHANGAA WASAMBAZAJI

Mrembo huyo alizidi kutiririka kuwa, anawashangaa watu wanaoeneza uvumi kuwa ametembea na Harmo, jambo ambalo si kweli.

“Nasikia watu wanasema kwamba, nimetoka kimapenzi na Harmonize, jambo ambalo siyo kweli. Ninamheshimu Harmonize kwa sababu ni mume wa mtu, yaani bora hata nitoke na camera man (mpigapicha) wake, lakini siyo yeye.

 

ALALA NAYE SIKU 3

“Na huwezi kuamini, nililala na Harmonize kwenye apartment moja kwa siku tatu, lakini hatukufanya jambo lolote, hata kuhusu hiyo ishu ya kufumaniwa naye siyo kweli, watu wanazusha tu,” alisema Nicole.

MENEJA WA HARMO SASA

Ili kujua kama uongozi umepokeaje suala la mwanamuziki wao kuchafuliwa hususan kwenye video hiyo iliyodaiwa kuwa ni ya fumanizi, Gazeti la IJUMAA lilimvutia waya meneja wa Harmo, Beauty Mmari ‘Mjerumani’ ili kusikia analizungumziaje.

 

Awali, alianza kwa kufoka, lakini baadaye mwanahabari wetu alimtuliza mzuka ndipo akasema watu wanaoeneza mambo hayo, wanataka tu kumharibia mwanamuziki wake.

 

“Hivi hamjui kama Harmonize na Sarah ni mke na mume? Jamani ile ni familia na kama familia, migongano katika ndoa ni kawaida, mimi hiyo video ambayo inasambaa mtandaoni kuwa Harmonize kafumaniwa nimeiona, lakini siyo kweli.

 

“Kwani Sarah hawezi kumfokea mume wake kama wamekoseana? Sasa kwa nini watu waseme anamfokea baada ya kumfumania? “Naomba sasa hivi tuangalie sana kazi anayoifanya na zaidi tumsapoti kwenye kutangaza albam yake ya Afro East, tuachane na mambo yasiyokuwa na maana kwa sababu hayasaidii kuufikisha muziki wetu mbali.

 

VIDEO NI YA MUDA…

“Hiyo video ni ya muda mrefu, ila watu wameamua tu kuivujisha sasa hivi ili kumharibia mwanamuziki wangu, kwa sababu mpaka tunavyoongea Harmonize hayupo Dar, sasa amefumaniwa lini?” Alihoji meneja huyo.

 

MAMBO YALIVYO

Licha ya ‘vurugu’ hizo mitandaoni ambazo zimetolewa ufafanuzi na wahusika, video ya Harmonize ambayo Nicole ameuza sura kama video queen, kwa sasa inakimbiza vilivyo kwenye mitandao mbalimbali ikiwemo YouTube na kujizolea mamilioni ya watazamaji.

Stori: MEMORISE RICHARD, Ijumaa

Leave A Reply