The House of Favourite Newspapers

Mrembo: Nipo na Mondi Miaka 3 Sasa!

0

“NDIYO, ni mwaka wa tatu sasa nipo naye katika mahusiano!” Ni kauli nzito iliyotolwewa na mrembo maarufu katika mitandao ya kijamii (sosholaiti) nchini Rwanda, Shaddy Boo alipoulizwa kama ana mahusiano ya kimapenzi na msanii maarufu nchini Tanzania, Nasibu Abdul au Diamond Platnumz.

Swali hilo limekuja baada ya ya Shaddy Boo kumuita Diamond ‘Soul of Mine’, jambo liloibua sintofahamu ya ni kipi hasa kinaendelea kati ya wawili hao.

Kupitia ukurasa wake wa Instagram, Shaddy Boo alitoa fursa kwa mashabiki wake kumuuliza maswali ndipo likaibuka suala la Diamond ambaye tangu ameachana na Tanasha Donna, Machi, 2020 hajaweka wazi mahusiano yake.

“Are you in love with Diamond Platnumz? Ameulizwa Shaddy Boo ambaye jibu lake lilikuwa ni; “Yes I am, we almost have 3 years now.”

Utakumbuka katika bethidei pati ya Diamond iliyofanyika Oktoba, 2017 katika Hoteli ya Hyatt Regency Dar es Salaam, Shaddy Boo alikuwa miongoni mwa watu walioalikwa na kuibua minong’ono ya hapa na pale.

Kama hiyo haitoshi, kwenye shoo ya Diamond aliyofanya Naivasha nchini Kenya, Januari, 2018, Shaddy Boo alikuwepo na kuna baadhi ya picha zilipigwa zikiwaonesha wakiwa chumbani pamoja na mpigapicha wa Diamond aitwaye Lukamba.

MREMBO HUYU NI NANI?

Gazeti la IJUMAA limechimba kwenye vyanzo vyake na kuelezwa kuwa, Shaddy Boo ni mrembo maarufu kwenye mitandao ya kijamii (sosholaiti) ambaye mwaka 2017 alidaiwa kunaswa hoteli moja jijini Dar akiwa na Diamond ambapo miongoni mwa mambo yaliyozua gumzo ni kitendo cha mrembo huyo kuonekana amevaa viatu vya wazi ambavyo awali vilikuwa vimevaliwa na Diamond wakati anaingia hotelini hapo.

Hata hivyo, wakati mrembo huyo akiondoka Tanzania, alinaswa na vyombo vya habari kwenye Uwanja wa Ndege wa Kimataifa wa Mwalimu Julius Nyerere jijini Dar na alipoulizwa juu ya uhusiano wake na Diamond alijibu;

“Nothing much is going on, we are just friends yeah! Aah! No! it’s not true, we are just friends. (Hakuna cha zaidi kinachoendelea, sisi ni marafiki wa kawaida tu yeah! Aah! Hapana! Si kweli, sisi ni marafiki wa kawaida tu)”

STORI; WAANDISHI WETU, DAR

Leave A Reply