Mrembo Shepu Biriani Atikisa Ukumbini

MREMBO mmoja aliyetajwa kwa jina moja la Mamuu, umbo lake limekuwa gumzo mjini kwa jinsi ilivyoonekana kutikisa ukumbini kutokana na kuwavutia baadhi ya mashabiki kwenye ukumbi wa burudani jiji Dar hata kusababisha kupachikwa jina la Mrembo Shepu Biriani.

 

Mwanahabari wetu alikutana na mrembo huyo Ijumaa iliyopita kwenye onesho la Msondo Music Band lililofanyika katika ukumbi wa Kisuma Mbagala ambapo alikuwa akifanya yake na kuwatoa udenda baadhi ya mashabiki na wanamuzki wa bendi hiyo.

 

Katika tukio hilo Mrembo Shepu Biriani wakati muziki ukikolea alikuwa akivamia steji na kutumia shepu yake kuwatikisia na kuwafanyanyia manjonjo wanamuziki wa bendi hiyo ambao walionekana kugombea kucheza naye.

 

Mrembo huyo naye alianza kuwapa staili mbalimbali kwa kuwanyongea nyonga zake kiufundi huku mashabiki wakimshangilia na wengine kusikika wakisema presha imeshuka, presha imepanda.

 

Manjonjo ya mrembo huyo hayakuishia kwa wanamuziki kwani kuna muda alionekana kuwageukia mashabiki waliionekana kummendea kucheza naye nao aliwarusha roho.

 

Kufuatia sakata hilo mwanahabari wetu alizungumza na mwanamuziki wa bendi hiyo Edo Sanga aliyeonekana kupenda staili ya uchezaji ya mrembo huyo ambapo alikuwa na haya ya kusema;

 

“Duuuh! Kaka yaani huyu mtoto figa yake ni balaa, kama yule biriani wa Tabata, nimecheza naye kidogo lakini nimehisi furaha kwa raha ya kucheza naye,”aalisema Edo ambaye ni muimbaji mkongwe wa bendi hiyo.

 

Mwanahabari wetu alimfuata mrembo huyo kwa nia ya kutaka kumhoji lakini alionekana kuwa bize kila alipotaka kumfanyia mahojiano na alionekana kutopendelea mahojiano.

STORI: RICHARD BUKOS, DAR

Toa comment