The House of Favourite Newspapers

MRISHO GAMBO APATA PIGO

MKUU wa Mkoa wa Arusha, Mrisho Gambo amepatwa na pigo la kuondokewa na dada yake mpendwa Bi. Mwajuma Gambo ambaye alifariki dunia jana Alhamisi, Oktoba 4, 2018 katika Hospital ya Taifa Muhimbili (MNH) jijini Dar es Salaam alikokuwa akitibiwa.


Kupitia Ukurasa wake wa Instagram, RC Gambo ameandika;

“Kwa masikitiko makubwa natangaza kifo Cha Dada yangu mpendwa Bi. Mwajuma Gambo (akitoka yeye ni mimi) kilichotokea Jana tarehe 04/10/2018 kwenye Hospital ya Muhimbili Dar Es Salaam.

 

“Mazishi yatakuwa siku ya Jumamosi tarehe 06/10/2018 Saa 6 Mchana kwenye makaburi ya MCHIKICHINI Ilala Dar Es Salaam.

 

Msiba upo nyumbani Kariakoo mtaa wa Mheza Karibu na Shule ya Sekondari ya Benjamini Mkapa. Mwaka huu tumepata mtihani mwingine. Kazi ya Mungu haina Makosa!.”

Inna Lillahi wa inna ilayhi raji’un.

=======

Maamuzi ya RC Makonda mbele ya watendaji TPSF Leo

Comments are closed.