The House of Favourite Newspapers

Mrisho Saleh; Mkimbizi Kutoka Kongo Anayeishi Marekani kwa Kuimba Qaswida

0

 

Wahenga wanasema mlango mmoja ukifungwa, basi mwingine unafunguka! Hiki ndicho kilichotokea kwa Mrisho Saleh, Mkongomani anayeishi Illinois nchini Marekani, baada ya kuondoka nchini kwao akiwa kama mkimbizi.

Akisimulia kupitia Kipindi cha Mapito, kinachorushwa na @255globalradio, Mrisho anaeleza kwamba kulitokea mapigano nchini kwao akiwa bado mdogo, tena akitokea katika familia maskini.

 

Kwa bahati nzuri, akawa miongoni mwa wakimbizi waliochaguliwa na Shirika la Kuhudumia Wakimbizi la UNHCR ambapo yeye na wenzake walipelekwa nchini Marekani.

Akiwa huko, ndiko alikogundua kipaji chake cha kuimba Qaswida, kazi iliyomfanya awe na uwezo wa kuendesha maisha yake vizuri kabisa.

Leave A Reply