The House of Favourite Newspapers

Mrithi wa Metacha Yanga Atajwa

0

RAZACK Siwa, Kocha wa Makipa wa Yanga, amesema kuwa wanaweza kumtumia kipa namba tatu, Ramadhan Kabwili katika mechi zilizobaki ikiwa ni pamoja na ya leo Jumapili dhidi ya Mwadui FC.

 

Mchezo huo wa Ligi Kuu Bara, unatarajiwa kuchezwa kwenye Uwanja wa Mkapa, Dar es Salaam.

 

Endapo leo Kabwili ataanza kikosi cha kwanza, basi utakuwa ni mchezo wake wa kwanza msimu huu wa 2020/21 ndani ya Ligi Kuu Bara baada ya Yanga kucheza mechi 30.

 

Kabwili ametajwa kuchukua nafasi ya kipa namba moja, Metacha Mnata ambaye amesimamishwa na uongozi kwa utovu wa nidhamu.

Akizungumza na Spoti Xtra, Siwa alisema kuwa kuna mechi ambazo zimebaki wanaamini watamtumia Kabwili ambaye hajapata nafasi ya kucheza.

 

“Nafikiri mechi bado hazijaisha, hivyo tumuombe Mungu, nafikiri kwa mechi ambazo zimebaki tunaweza kumuona Ramadhan Kabwili akianza kwani huwa ninafundisha kila mchezaji kupata nafasi ya kucheza.

 

Ninarudia kusema kuwa mapumziko tuliyopata wakati ule wa timu ya taifa yametufanya tuwe imara, hivyo tunahitaji kupata matokeo chanya katika mchezo wetu dhidi ya Mwadui FC,” alisema Siwa.

 

Kuelekea mchezo wa leo, Kabwili alisema: “Ninaamini kwamba mazoezi ni magumu kuliko mechi, hivyo kwangu nipo tayari, tusubiri tuone kocha atampanga nani kati yetu, sisi sote ni timu moja, tunahitaji ushindi.”

Kwa upande wa Frederick Masombola, Kocha Msaidizi wa Mwadui FC, alisema: “Msimu huu tumecheza mechi mbili na Yanga, ile ya 5-0 (ligi kuu), na wa pili tulifungwa 2-0 (Kombe la FA), hivyo tumejipanga na wachezaji wapo tayari kisaikolojia.”Mussa Mbissa, nahodha wa Mwadui FC, alisema

WAANDISHI WETU,DAR

Leave A Reply