The House of Favourite Newspapers

MRITHI WA MONDI NI HUYU ?

Zarinah Hassan ‘Zari The Boss Lady’

 MAMBO ni moto, huko Instagram kumechafuka watu wanamsaka kwa udi na uvumba mrithi wa Nasibu Abdul ‘Diamond Platnumz’ kwa mzazi mwenzake Zarinah Hassan ‘Zari The Boss Lady’ ambapo safari hii kawekwa mwanaume anayedaiwa kuwa ndiye mhusika. Wananzengo wa Instagram wamempongeza jamaa huyo ambaye jina lake bado halijapatikana kwa kusema anaonekana ni mtu mzuri tofauti na Mondi.

“Wanaume wa aini hii ni wazuri sana… kama namuona Mondi anavyoteseka,” alichangia Kidoboy. Licha ya mashabiki kuonekana kuwa na shauku ya kutaka kumjua mrithi wa Mondi, Zari bado hajaamua kumwanika moja kwa moja mrithi huyo.

Comments are closed.