The House of Favourite Newspapers

Msaga Sumu, Man Fongo Jukwaa Moja IDD EL FITR

WAKALI wawili wasioshikika kunako gemu ya Muziki wa Singeli, Man Fongo na Msaga Sumu wanatarajiwa kukutana jukwaa moja kwa mara ya kwanza Sikukuu ya Idd el Fitr ndani ya Uwanja wa Taifa wa Burudani, Dar Live uliopo Mbagala- Zakhem jijini Dar katika bonge moja la shoo linalota-mbulika kama Usiku wa Nani Atazima?

 

Akizung-umza na Risasi Vibes, Meneja na Mratibu wa Dar Live, Rajab Mteta ‘KP Mjomba’ alisema kuwa, kwa muda mrefu mashabiki walikuwa na kiu ya kuwaona Man Fongo na Msaga Sumu wakifanya shoo ya pamoja jukwaani baada ya kila mmoja kuwa juu.

 

“Hakuna asiyefahamu kama Man Fongo na Msaga Sumu ni wasanii wakali ambao mara kwa mara kila mmoja amekuwa yupo juu ya mwenzake. Baada ya kushindana nje ya jukwaa kwa muda mrefu Dar Live tumew-aletea moja kwa moja ambapo Sikukuu ya Idd unavyofi-kiria wewe nani atazima mbele ya mwenzake?” Alisema KP.

 

Ngoma zao sasa!

KP aliongeza kuwa, usiku huo utakuwa wa bandika bandua ambapo kila mmoja atahakikisha anaondoka na kijiji.

“Pata picha ukimsikia Msaga Sumu na Ngoma ya Unanitega Shemeji huku upande wa pili msikie Man Fongo na Ngoma ya Hainaga Ushemeji, yaani usiku huo ni kushuhudia nani atazima,” alisema KP.

 

 

Wakali wengine wapo

KP aliongeza pia, mbali na uwepo wa wakali hao wa Singeli, jukwaa litashambuliwa pia na wakali wa Bongo Fleva wasioshikika, Young Killer na Young Dee ambapo kila mmoja atamuonesha mwenzake nani zaidi.

 

“Young Killer anazo ngoma kibao ambazo zitawasimamisha mashabiki wengi, ngoma kama vile Kumi na tatu (13), True Boya, Hujanileta, Popote Kambi, How we Do, Dear Gambe, Jana na Leo, Umebadilika, Mrs Superstar na nyingine kibao.

 

“Upa-nde wa Young Dee naye anazo ngoma kibao kama vile Hands Up, Bongo Bahati Mbaya, Kiben10, Tunapeta, Kiutaniutani, Tunapeta na nyingine nyingi,” alisema KP. Burudani kwa watoto Shoo ya mapema itakuwepo mapema kuanzia asubuhi kwa burudani kabambe ya watoto.

 

“Tuta-kuwa na michezo mingi ya watoto kama vile kuogelea, kucheza na baiskeli spesho, kuvu-tana ka-mba kupanda ndege spe-sho pamoja na kuogelea huku burudani ya sarakasi na kucheza muziki ikitolewa na Wakali Dancers,” alimaliza KP.

 

Burudani zote hizo zinapatikana kwa mtonyo kiduchu wa buku 7 tu getini wakati shoo nzima ya watoto ikiwa kwa kiingilio cha buku tu.

Risasi Vibes.

Comments are closed.