KAMANDA wa Polisi Mkoa wa Dodoma, Giles Mroto amesema kuwa jeshi hilo limefanya operesheni ya kusaka wahalifu na kufanikiwa kunasa gari moja lililokuwa limebeba malighafi ya mabati.
Hilo lilitokea jana Machi 2, 2018 ambapo Mroto alisema msako huo ni moja ya kutimiza adhima ya jeshi hilo kutokomeza uhalifu mkoani Dodoma. Alieleza kuwa wamefanikiwa kukamata wahalifu wakiwemo, wasafirishaji mali za magendo na watengenezaji bima feki.
Aidha, jeshi hilop linawashikilia wahamiaji haramu wawili raia wa Rwanda pamoja na watoto 20 wa mitaani wenye umri kati ya miaka 7 hadi 15 ambao wamekuwa wakitumiwa na wahalifu kuiba vifaa mbalimbali vya magari.
Tutumie video ya tukio lolote ambalo limetokea hapo ulipo kupitia WhatsApp 0753 715 779 tutakulipa mkwanja papo hapo.
Comments are closed.