The House of Favourite Newspapers

Msama Ampongeza JPM Kuwatoa Babu Seya, Papii Kocha Gerezani

Mkurugenzi wa Kampuni ya Msama Promotion, Alex Msama akizungumza na waandishi wa habari.

 

SIKU chache tangu kuachiwa kwa wasanii, Nguza Viking ‘Babu Seya’ na mwanaye Johnson Nguza ‘Papii Kocha’ waachie huru na Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. John Magufuli, Mkurugenzi wa Kampuni ya Msama Promotion, Alex Msama amempongeza rais kwa hatua hiyo akisema hakika anapaswa kushukuliwa.

Msama ambaye pia aliwahi kuwa mjumbe wa bodi ya Baraza la Sanaa Tanzania (BASATA) akizungumza na waandishi wa habari ofisini kwake amepongeza kwa dhati hatua hiyo ya rais akisema amefanya jambo la kibinadamu na si tu hilo bali ametekeleza pia agizo la mwenyezi mungu la kusamehe.

“Watanzania wamefurahi sana kwa jambo alilolifanya mheshimiwa rais wetu Dkt John Pombe Magufuli la kutoa msamaha kwa mwanamziki mkongwe na maarufu Babu Seya yeye pamoja na familia yake, ikumbukwe wanamziki hao walihukumiwa takribani miaka 13 iliyopita na wametumikia kifungo hicho na kwa hiyo, rais amefanya jambo la kihistoria”. alisema Msama

Msama amerudia wito wake wa kuwataka watu wanaonyonya kazi za wasanii kuacha mara moja kwani zoezi la kuwakamata bado linawale wote wanaohusika kwa kufanya hivyo na kuwafikisha mahakamani linaendelea nchi nzima n kuwataka wananchi kununua kazi hizo zenye nembo ya TRA kwani kutapelekea wasanii kunufaika na kazi zao pia serikali kujipatia kodi pia.

Hata hivyo Msama amemuomba rais kutekeleza ahadi yake aliyowapa pale alipokutana nao Ikulu ya kupambana na wanyonyaji wa kazi za wasanii ili mwisho wa siku wasanii kote nchini wafaidike na kazi zao.

 

NA DENIS MTIMA/GPL

Comments are closed.