The House of Favourite Newspapers

Msando Awalipua UVCCM Mbele ya Magufuli (Video)

Wakili Alberto Msando akiongea kwenye Mkutano wa UVCCM Taifa, Dodoma, leo.

WAKILI Alberto Msando, ambaye alijiunga na Chama Cha Mapinduzi (CCM) akitokea chama ACT-Wazalendo, leo akiongea kwenye mkutano wa UVCCM Taifa, unaoendelea Dodoma, amefunguka na kuwachana vijana wa chama hicho (UVCCM) baada ya viongozi wake aliodai walimdanganya Mwenyekiti wa CCM,  John Pombe Magufuli juu ya idadi wa vijana wao.

Albert Msando aliomba nafasi kwa Rais Magufuli ili aweze kuwasema vijana hao wa CCM baada ya moja ya taarifa yao kusema wapo vijana wa CCM zaidi ya milioni sita,  jambo ambalo linapingana na taarifa zao wenyewe.

“Nimeazima taarifa ya utekelezaji na mpango mkakati naona mmesema kwamba UVCCM mpo milioni sita.  Je, ni kweli? Kama vijana mtakuwa mnafanya mambo kama haya, tutakuwa na nchi ya hovyo sana na chama cha hovyo sana.  Mmeandika takwimu zinazoonyesha kuwa idadi ya vijana wenye umri kati ya 14 na 35 ni asilimia 34 ya watu wote nchini. Mara tu baada ya ukurasa wa nane, ukurasa wa tisa mmeandika kundi la vijana ni kubwa, takwimu zinaonyesha sasa wamefikia asilimia 65 ya idadi ya watu nchini.  Ina maana hatujijui tupo wangapi?” alihoji Msando

Akiendelea kuonyesha mapungufu hayo, Msando alisema:

“Kwenye kitabu hiki mmemwambia Rais Magufuli kuwa vijana wa UVCCM mnafika milioni sita lakini kwenye jedwali la kweli mmeandika idadi ya vijana wa UVCCM kila mkoa tangu 2013 hadi 2017 jumla walio hai ni milioni moja laki sita,  wasio hai ni laki nne.  Sasa kwa nini mmdanganye Rais? Tukafanye kazi na hizi ndiyo takwimu zenu,  sasa hivi mnamwambia Rais tunakaribia milioni sita.  Mnataka Rais aondoke akiwa na picha ya kuwa mpo zaidi ya milioni sita wakati mpo milioni moja laki tano?  Jamani hatuendi hivyo,  tunakata CCM mpya ya vijana wachapa kazi,  Wanachama wote ambao hawapo hai warudi, tupate wanachama wapya, ” alisema Msando.

Comments are closed.