The House of Favourite Newspapers

Msanii alewa!

0

MSANII ALEWA (1)

Msanii wa filamu za Bongo, Glasnost Kalinga akilia wakati marafiki zake wakitaharuki.

Mayasa Mariwata Na Shani Ramadhani

MSANII wa filamu aliyefahamika kwa jina la Glasnost Kalinga hivi karibuni alipata aibu ya aina yake baada ya kulewa na kushindwa kutembea.

Msanii huyo alinaswa na kamera yetu maeneo ya Afrikasana, Sinza saa 6 usiku ambapo alionekana akiwa amelala chini huku marafiki zake wakijaribu kumkokota bila mafanikio.

MSANII ALEWA (5)…Akigalagala

Akizungumnza na Ijumaa katika eneo la tukio, mmoja wa marafiki wa msanii huyo aliyeomba jina lake lisiandikwe gazetini alidai kuwa, hakuna chochote kibaya kilichompata ila alizidiwa na pombe.

MSANII ALEWA (4)…Wote wakishangaana

“Hana tatizo, ni pombe tu ndiyo maana yuko katika hali hii. Tulitoka vizuri viwanja tukiwa ndani ya Bajaj lakini tulipofika hapa na kushuka tukashangaa mwenzetu kasinzia, tulipomuamsha akaonekana hajitambui, aliposhuka ndiyo kashindwa kutembea,” alisema shosti huyo.

MSANII ALEWA (3)Hali ya sintofahamu ikiendelea

Baada ya paparazi wetu kunasa tukio hilo usiku, kesho yake asubuni alimpigia simu Glasnost na kumuuliza ilikuwaje ambapo alisema kwa kifupi kuwa hajui kilichotokea kwani ndiyo alitoka kuamka.

MSANII ALEWA (2)…Wakiondoka eneo hilo

“Ndiyo nimeamka hapa, ila kwa kweli sijui hata kilichotokea jana ,” alisema msanii huyo ambaye ameonekana kwenye filamu mbalimbali kama vile Bikira, Mwadawa na nyinginezo.

JIUNGE NA GLOBAL BREAKING NEWS!

globalbreakingnews.JPG

Leave A Reply