The House of Favourite Newspapers

Msanii Aliyeshika Kichwa cha Rais Trump Afukuzwa Kazi CNN

0

Msanii mchekeshaji raia wa Marekani, Cathy Griffin (57) aliyeonekana live kupitia kipindi cha runinga kinachorushwa na Kituo cha CNN akiwa ameshika kinyago kinachofanana sana na kichwa cha Rais Donald Trump huenda akashtakiwa kutokana na kile kilichotajwa kama kuvuka mipaka ya uhuru wa habari.

Msanii huyo alionekana akiwa amebeba kinyago cha Rais Trump akiwa amekatwa kichwa, jambo ambalo limezua hasira miongoni mwa watu wengi wakiwemo wapinzani na wafuasi wa Trump nchini Marekani.
Baada ya Tukio hilo Kituo cha Runinga cha CNN kilitangaza kumfukuza kazi msanii huyo na kukifuta kipindi chake mara moja.

Baadhi ya watu maarufu nchini Marekani akiwemo Rais Trump mwenyewe, wamekilaani kitendo hicho na kusema ni dhihaka na udhalilishaji kwa familia za wanajeshi na baadhi ya waandishi wa habari wa Marekani waliochinjwa na Kundi la Kigaidi la ISIS.

Taarifa iliyotolewa na Idara ya Ulinzi wa Rais nchini marekani (Secret Service) imesema uchunguzi umekamilika na wanajiandaa kumfikisha mahakamani Cathy Griffin.
Kathy Griffin holds up Donald Trump’s decapitated head in new photo shoot

Leave A Reply