Msanii Apenyeza Bongo Fleva Australia

Msanii wa Bongo Fleva, Simon Masanja ‘Simorix The General’ ambaye ni Mtanzania anayeishi nchini Australia ameanza rasmi harakati za kuupenyeza muziki huo nchini humo.

Akizungumza na mtandao huu leo, Simorix amesema tayari ana nyimbo ambazo ameshazipika na kilichobakia ni kuzisogeza kwa mashabiki tu nchini humo.

“Nina kiu ya kupeperusha bendera yetu Australia kupitia Bongo Fleva ambayo kiukweli imeanza kupenya na kukubalika. Kwa hiyo nina nyimbo kadhaa ambazo nitaziachia kabla mwaka haujaisha. Kikubwa ninaomba mashabiki wazipokee maana zote ni hit,” anasema Simorix General.

Ameongeza kuwa mipango yake ya baadaye ni pamoja na kuandaa matamasha na timu yake kwa sasa akili kubwa nimewekeza katika kutangaza kazi zake nchini humo.

Simorix The General mpaka sasa anatamba na kibao chake cha Tunapiga Bao akiwa amefanya cover ya Wimbo wa Shettah wa Hatufanani huku beats ikiwa imetengenezwa na prodyuza Kimambo na Director ni Daniele Cernera kutokea Australia. Beat aliyotumia Simorix ndiyo beat iliyotumiwa na mwanadada Nandy na Shetta.

Na Neema Adrian


Loading...

Toa comment