The House of Favourite Newspapers

Msanii wa Bongo Fleva Nandy Alijisikia Vibaya Kumkana Mwanaye Pindi Alipohojiwa

0
Msanii wa bongo fleva Nandy akiwa na mume wake mtarajiwa Nenga ambaye pia ni msanii wa bongo fleva

Nandy The African Princess; ni msanii mkubwa wa kike nchini Tanzania ambaye anasema kuwa, amefikia hatua ya kuuanika ujauzito wake kwa sababu alichoka kumkana mwanawe kila alipokuwa akihojiwa.

 

Nandy au Mama Nenga anasema; “Nadhani tulitaka kuweka wazi ujauzito pamoja na projekti yangu nyingine. Lakini pamoja na mambo yote hayo, bado nimebaki kuwa msanii na maisha lazima yaendelee. Siwezi kuendelea kuficha ujauzito kila wakati.

 

“Ujauzito ni baraka na unavyojua kuna watu wengi wanahangaika kutarajia kuwa wazazi, tunawaombea wote, kwa kazi zetu sikuweza kujificha tena kwani kazi bado zinanihitaji, nachukia kila mtu.

 

“Wakati nafanya mahojiano na kumkana mtoto wangu, nilikuwa nikijisikia vibaya huku nikidanganya kuwa sina mimba.”

Leave A Reply