The House of Favourite Newspapers

MSD Yaboresha Huduma za Kiuchunguzi na Maabara

0

 

Mkurugenzi Mkuu wa MSD, Bw. Mavere Tukai

BOHARI ya Dawa (MSD) imeendelea kufanya Maboresho na mageuzi upande wa huduma za kichunguzi na maabara nchini, kwa kuleta vifaatiba vya kisasa, vyenye kutumia teknolojia ya kisasa ili kuenenda sambamba na mabadiliko ya teknolojia ulimwenguni.

 

Hayo yamefafanuliwa na Mkurugenzi Mkuu wa MSD, Bw. Mavere Tukai akifafanua kwa undani, wakati wa mahojiano maalum

 

Maboresho haya yamefanyika kwenye ngazi zote za vituo vya kutolea huduma za afya nchini, kuanzia vituo vya afya vya msingi hadi Hospitali za kitaifa.

Vifaa vya Maabara

Aidha Bw. Mavere amebainisha kuwa MSD imenunua mashine mbalimbali za X-Rays, Mashine za kupima ni namna gani maini, damu na figo zinavyofanya kazi pamoja na mashine ya CT scan.

Leave A Reply