The House of Favourite Newspapers

Dkt Abbas: “Wanaokosoa Miradi ya Serikali ni wa kupuuzwa”

Mkurugenzi wa Idara ya Habari (MAELEZO) ambaye pia ni Msemaji Mkuu wa Serikali, Dkt. Hassan Abbas (kushoto) akiongea jambo  na Mkurugenzi Mtendaji wa Makampuni ya Global Group na mhamasishaji maarufu Afrika Mashariki na Kati, Eric Shigongo, leo katika ofisi za Global Group Sinza-Mori jijini Dar es Salaam akiwa katika ziara yake ya kikazi katika vyombo vya habari.

 

MKURUGENZI Mkuu wa Idara ya Habari (Maelezo) na Msemaji Mkuu wa Serikali Dkt. Hassani Abbas, mapema leo amepata fursa ya kutembelea ofisi za Global Group na  kuteta mambo mbalimbali na Mkurugenzi Mkuu wa Makampuni ya Global Group, Eric Shigongo,  na baadaye akapata fursa ya kufanya mahojiano mafupi na kituo cha Global TV Online.

Dkt. Abbas akifafanua jambo katika studio ya Global TV Online.

Mkurugenzi huyo pia alipata nafasi ya kubadilishana mawazo na baadhi ya wafanyakazi wa kampuni hiyo yenye ofisi zake zilizoko Sinza-Mori jijini Dar es Salaam.

Pia amefanya mahojiano na Global Tv Online na kuzungumzia mipango ya serikali kwa mwaka 2019 ikiwemo ujenzi wa vituo vya afya 69 nchini na ujenzi wa reli ya kisasa itakayotumia treni ya umeme.

Shigongo  akimweleza jambo Dkt. Abbas katika studio ya Global Radio ambayo bado haijazinduliwa.

Kuhusu Watu wanaokosoa miradi mikubwa ya maendeleo ikiwemo ununuzi wa ndege, Dk Abbas amesema hao ni wa kupuuzwa na kinachofanyika sasa ni kutekeleza ahadi ya serikali ya awamu ya Tano.

Katika hatua nyingine Dk Abbas amesema ataendelea na ziara zake katika maeneo mbalimbali nchini lengo ni kuwaeleza wananchi yanayofanywa na serikali pamoja na kupokea kero na kuziwasilisha kwenye taasisi husika.

Meneja Mkuu wa Global Publishers, Abdallah Mrisho (kulia) akiongozana na Dkt.  Abbas  na Shigongo wakielekea Studio ya Global TV Online.
Ni wakati wa kuagana…

 

HABARI/PICHA: MUSA MATEJA 

JIUNGE NA FAMILIA YA GLOBAL TV UPANDE MTANDAO WA MAFANIKIO

Bofya hapa kujiunga na familia ya Global TV Club ==> Global TV Family Club

Comments are closed.