Msemaji wa Serikali, Polepole Wafunguka Ajali ya Lori Moro

MKURUGENZI  wa Idara ya Habari (Maelezo) ambaye pia ni Msemaji Mkuu wa Serikali, Dkt Hassan Abbas, na Msemaji wa Chama Cha Mapinduzi (CCM) Humphrey Polepole, leo Agosti 10, 2019, wametoa kauli zao kupitia akaunti zao za Twitter,   kuhusiana tukio la lori lenye kubeba mafuta kupinduka mjini Morogoro eneo la Msamvu na baadaye kulipuka na kusababisha vifo vya watu zaidi ya 60 na kujeruhi 70.

Wengi wa waliofariki ni wale waliokuwa wakichota mafuta kutoka katika lori hilo.

Katika akaunti yake huo, Dkt. Abbas amesema:

”Tumepokea kwa masikitiko taarifa kuhusu ajali ya lori la mafuta, Morogoro, iliyosababisha moto na kuunguza watu kadhaa. Mkuu wa Mkoa na timu za uokoaji wanaendelea kukabiliana na hali katika eneo la tukio. Taarifa kamili kuhusu idadi ya vifo na majeruhi itatolewa badae. Tunaendelea kutoa wito kwa wananchi kukaa mbali na eneo la ajali hasa yanapohusika magari au vyombo vingine vya usafiri vilivyobeba vitu vinavyoweza kuripuka kama mafuta.”.

Naye Polepole amesema:
Uongozi wa @ccm_tanzania umepokea kwa mshtuko taarifa za ajali ya lori huko Msamvu Morogoro ambayo imegharimu maisha ya watanzania. Rai yetu kwa Jeshi la Polisi na Zimamoto ni kuendelea kutoa elimu na kusimamia utii wa sheria. Tunatoa pole kwa wafiwa na majeruhi kupona haraka

 


Loading...

Toa comment