Mshambuliaji wa mabao John Bocco Aipa Jeuri JKT Tanzania
UWEPO wa mshambuliaji wa mabao John Bocco ndani ya kikosi cha JKT Tanzania umeipa jeuri timu hiyo kwa kutuma salamu kwa makipa wa timu pinzani.
Bocco mshambuliaji bora wa muda wote ndani ya Bongo akiwa amefunga zaidi ya mabao 100 kwenye ligi ni ingizo jipya ndani ya timu hiyo akitokea Simba ambapo hakuongeza mkataba baada ya kandarasi yake kugota mwisho.
Masau Bwire, Ofisa Habari wa JKT Tanzania amesema: “Kwa sasa hakuna muda wa kupoteza tunaamini kwamba makipa watapata tabu ukizingatia tuna mshambuliaji wa mabao. Tupo tayari na tunafanya maboresho makubwa kwenye kikosi.”
Julai 10 Bocco alitambulishwa kuwa ni mchezaji mpya ndani ya kikosi cha JKT Tanzania hivyo atakuwa hapo kwa msimu wa 2024/25.