Mshambuliaji wa Yanga Sadney Urikhob Atua Nchini

Mshambuliaji wa kimataifa wa Namibia Sadney Urikhob amewasili tayari Tanzania kwa ajili ya kujiunga na klabu ya Yanga.

Urikhob ametua nchini na sasa ataelekea mjini Morogoro kujiunga na wenzake kwa ajili ya kambi maalum inayoendelea.

Mshambuliaji huyo alishamalizana na Yanga kwa kuingia nao mkataba wa miaka miwili.

Pro huyo amepokelewa na viongozi wa Yanga katika Uwanja wa Ndege na sasa kinachofuata ni kambi ya moja kwa moja Morogoro.

Toa comment