The House of Favourite Newspapers

MSHANGAO HAUSIBOI ANASWA LIVE AMEVAA NGUO ZA BOSI WAKE WA KIKE

HEE! Ndivyo unavyoweza kupata mshangao baada ya kijana mmoja aliyefahamika kwa jina la Jack, Mkazi wa Mikocheni A jijini Dar, kupata fedheha kubwa kwa kunaswa akiwa amevaa nguo za bosi wake wa kike na kutanulia nazo mitaani. 

 

Akisimulia tukio lilivyokuwa, bosi wa kijana huyo aliyejitambulisha kwa jina moja la Doi, alisema alikwenda nyumbani anapoishi na kumuomba kumsaidia kufanya kazi kama hausiboi na kwamba atamlipa mwisho wa mwezi.

“Unajua huyu kijana nilikuwa namuona mara nyingi anakuja kwenye nyumba ambayo nimepanga, kuna watu anawafahamu sasa kuna siku alinifuata na kuniomba nimpe kazi ya kuwa ananifanyia usafi na kunifulia, kitu ambacho nilimkubalia na kujua ni kijana tu ambaye anafahamika eneo ninaloishi,” anasimulia Doi.

 

Doi anasema kwa sababu alikuwa ameshamuamini akawa anamuachia ufunguo wa nyumbani kwake hivyo akimaliza kufua anakunja nguo na kuziweka ndani.

 

“Wala nilikuwa sijali na hata akili ya kuniambia nikague nguo zangu mara anaponifulia sikuwa nayo. Kuna siku nilimpa nguo azikunje ambazo zilifuliwa na mtu mwingine kisha nikaenda kwenye mizunguko yangu, niliporudi jioni wakati nataka kuzipanga nikagundua shati moja la drafti hamna.

“Mwanzoni nilivyompigia simu alikataa lakini nilipompa vitisho alikubali nikamwomba alete na nguo nyingine alizoiba sitamfanya kitu, akakubali ambapo alileta na nguo zangu ambazo nilisahau hivyo nikamsamehe, nikaendelea kumpa nguo za kufua kama kawaida,” anaendelea kusimulia Doi.

 

Baada ya kumpa msamaha huo, siku kama nne mbele Doi akiwa anaenda kazini alipishana na kijana huyo akiwa amevaa suruali yake ya jinzi ya kubana ambayo anadai aliitafuta sana mpaka akagombana na rafiki yake kwa kudhani aliichukua.

“Ikanibidi kushuka kwenye gari yangu kwa haraka na kuanza kumrukia kwa kumchapa vibao huku baadhi ya watu wengine wakinisaidia kumshika mpaka kituo kidogo cha polisi cha Mikocheni A na kumuweka selo kwa muda na kupewa karatasi ya taarifa ya polisi yenye namba OB/RB/3094/2019 kisha akapelekwa kituo kikubwa cha Polisi cha Oysterbay.

 

Mpaka gazeti hili linakwenda mtamboni haikufahamika kilichoendelea licha Doi kueleza kuwa, anajua kijana huyo amevaa nguo zake sana hivyo atambana ili azirudishe kisha anaweza kumsamehe na kuachana naye mazima.

Comments are closed.