The House of Favourite Newspapers
gunners X

Mshindi wa Airtel Trace apata ujuzi mpya toka kwa Akon

Pic 2Mkurugenzi wa mawasiliano wa Airtel Bi Beatrice Singano Malya akiongea na mshindi wa Airtel Trace Music Stars Nalimi Mayunga wakati alipotembelea ofisi za Airtel mara baada ya kuwasili kutoka nchini Marekani alipoenda kurekodi video yake na kupata mafunzo kutoka kwa mwanamuzi nguli Akon. Safari hii ni moja kati ya zawadi ya kufanya video na Akon pamoja na mafunzo alizipata mara baada ya kuibuka mshindi wa shindano hilo Afrika .

Pic 4Mshindi wa Airtel Trace Music Stars Nalimi Mayunga akiongea na waandishi wa habari wakati alipotembelea ofisi za Airtel mara baada ya kuwasili kutoka nchini Marekani alipoenda kurekodi video yake na kupata mafunzo kutoka kwa mwanamuzi nguli Akon. Akishuhudia ni Mkurugenzi wa mawasiliano wa Airtel Bi Beatrice Singano Malya

Pic 5Mkurugenzi wa mawasiliano wa Airtel Bi Beatrice Singano Malya akifurahia jambo na mshindi wa Airtel Trace Music Stars Nalimi Mayunga wakati alipotembelea ofisi za Airtel mara baada ya kuwasili kutoka nchini Marekani alipoenda kurekodi video yake na kupata mafunzo kutoka kwa mwanamuzi nguli Akon.Pic 3Mkurugenzi wa mawasiliano wa Airtel Bi Beatrice Singano Malya akisalimiana na kumpongeza mshindi wa Airtel Trace Music Stars Nalimi Mayunga wakati alipotembelea ofisi za Airtel mara baada ya kuwasili kutoka nchini Marekani alipoenda kurekodi video yake na kupata mafunzo kutoka kwa mwanamuzi nguli Akon

Dar es Salaam, 1st December 2015, Mshindi wa Airtel Trace Music Stars Nalimi Mayunga amerudi nchini kutoka Marekani alipoenda kwa ziara ya wiki moja kwaajili ya kurekodi video yake na kupata mafunzo kutoka kwa mwanamuziki nguli Akon

Nalimi Mayunga alisema hii imekuwa nafasi ya pekee maishani mwake na anapenda kuwashukuru sana Aitel na Trace kwa kupatia fulsa hii.

“Nimefurahia muda niliokaa mjini Losa Angeles Marekani na kupata wakati mzuri wa kumtembelea Akon nyumbani kwake na kufanya rekoding ya video na kupata mafunzo ya musiki alisema.

Nalimi aliongeza kwa kusema fursa hii imenipa mwanga zaidi katika namna ya kufikiri na kujipanga ili kuzifikia ndoto zangu katika tasinia ya muziki. Nimejifunza mambo mengi sana kupitia mafunzo niliyopata kutoka kwa Akon ikiwemo jinsi ya kukabili jukwaaa, namna ya kuchezea sauti yangu, mafunzo ya sauti, namna ya kuandika na kutunga nyimbo na jinsi ya kuinua muziki wangu na kukuza kipaji change kwa ujumla”

Nalimi aliyejawa furaha pia alieeleza shauku aliyonayo ya kutoa kibao hicho kwa kushirikiana na Akon na kusema kwamba kitafungua milango yake katika ulimwengu wa muziki kwani amepata nafasi ya kuingia na kurekodi wimbo wake kwenye studio ya universal Hollywood yenye vifaa vya kisasa na vyenye technologia ya juu“ na uhakika video yangu itakuwa moja kati ya video bora za muziki sokoni na hivyo nawashurukuru sana mashabiki wangu, watanzania kwa ujumla kwa kunipigia kura na kuniwezesha kufika hapa nilipo leo”

Akieleza zaidi kuhusu safari ya Mayunga, Mkurugenzi wa mawasiliano wa Airtel Bi Beatrice Singano Malya alisema “ tunafurahi kuwa sehemu ya kubadilisha maisha ya vijana wengi akiwemo Nalimi Mayunga.

Tunaamini mayunga atakuwa ni mfano utakaowavutia vijana wengi kuzifikia ndoto zao. Tunapenda kuwahamasisha vijana wengi zaidi kushiriki katika program zetu nyingi zenye lengo la kuwawezesha kufikia malengo yako kama vile Airtel Fursa, Airtel Rising Stars, Airtel Trace Music Stars na nyingine nyingi .

Msimu wa pili wa shindano kubwa la muziki la Afrika la Airtel Trace Music Stars mwaka 2016 linategemea kuzinduliwa rasmi mwanzoni mwa January 2016, tunatoa wito kwa vijana wengi kushiriki pindi shindano hili litakapotangazwa rasmi. Aliongeza Mallya

Comments are closed.