Mshindi wa Championi achekelea mkwanja

MSHINDI wa shindano linaloendeshwa na gazeti namba moja la michezo Championi, Emmanuel Daud, amechekelea kupewa zawadi yake ya ushindi baada ya kujishindia mkwanja aliopewa makao makuu ya Global Group, Sinza Mori.

Shindano hilo ambalo ni maalumu kwa ajili ya wasomaji wake lenye lengo la kurejesha kidogo ambacho wanakipata, limeanza kubamba baada ya hadi sasa kutoa washindi 14 ambao wamejinyakulia zawadi zao bila longolongo.

Akizungumza mara baada ya kupewa zawadi yake ambayo ni shilingi 10,000, Daud alisema kuwa furaha yake haielezeki kwani amekuwa na kawaida ya kununua gazeti la Championi muda wote bila kujali kuna shindano kutokana na ubora wake.

“Championi ndiyo gazeti langu la muda wote hivyo kama utahitaji kujua nimeshiriki mara ngapi, nasema ni mara zote, huwa silikosi gazeti na nitaendelea kununua kutokana na ubora wake na habari zake zote ni za uhakika.

“Nakaa Kinondoni kwa hapa Dar es Salaam, hivyo nawashauri wasomaji wengine waendelee kununua kwa wingi zawadi zipo nyingi na za tofauti hivyo wawe na imani na shindano hili ni la kweli kabisa,” alisema Daud.

SAID ALLY, Dar es Salaam

Toa comment