Mshindi wa M-Bet alamba mil.28
Mkurugenzi wa Kampuni ya M-BET, Dhiresh Kaba (kulia), akimkabidhi mfano wa hundi mshindi wa zaidi ya milioni 28, Robert Mwangasame katika Ukumbi uliopo ndani ya Mbeya Hoteli jijini Mbeya mapema leo.
Mshindi wa milioni 28, Robert Mwangasame (kushoto), akifurahia kwa pamoja na Mkurugenzi wa M-BET, Dhiresh Kaba wakati wa makabidhiano na mfano wa hundi hiyo.
Mkurugenzi wa Kampuni ya M-BET, Dhiresh Kaba akiongea jambo muda mfupi baada ya makabidhiano hayo kukamilika.
Mkurugenzi wa Bodi ya michezo ya kubahatisha nchini Tarimba Abbas (kushoto), akimkabidhi hundi hiyo mshindi wa zaidi ya shilingi milioni 28, Robert Mwangasame (kulia), huku Mkurugenzi wa M-BET, Dhiresh Kaba (katikati), akinyanyua mkono wa pongezi, mapema leo ndani ya Ukumbi uliyopo katika Hoteli ya Mbeya.
Kaba (wa kwanza kushoto), akiwa kwenye kikao cha Waandishi wa habari muda mfupi kabla ya makabidhiano hayo kufanyika.
Baadhi ya waandishi wa habari kuotoka vyombo Mbalimbali vya habari hapa mjini Mbeya (kulia), wakifuatilia kwa makini makabidhiano hayo.
MSHINDI wa michezo wa kubahatisha ambaye ni Mwalimu wa shule ya Sekondari ya Viwawa Mbozi Mkoani Mbeya Robart Mwangasame, hatimaye amekabidhiwa kitita cha zaidi ya shilingi milioni 28 baada ya kushiriki bahati Nasibu kwa njia ya kubet inayoongozwa na Kampuni ya M-Bet iliyo chini ya Mkurugenzi wake Dhiresh Kaba.
Makabidhiano hayo yalifanyika kwenye Ukumbi WA Mbeya Hotel uliopo mjini hapa mapema leo.
Akizungumza kwa furaha muda mfupi baada ya kukabidhiwa fedha hizo Mwangasame alisema kuwa, amefurahishwa na ushindi huo mkubwa ambao kiwastani hakutarajia kama angeweza kuibuka kidedea, kwani alitumia shilingi elfu moja tu kucheza na kushinda kitita hicho.
“Kiukweli naweza kusema kampuni ya M-Bet, itakuwa imeinua maisha yangu kwa kiasi kikubwa kuanzia leo, maana nakumbuka Oktoba 18 mwaka huu ndiyo siku niliyopigiwa simu na Mkurugenzi wa M-BET, bwana Dhiresh Kaba akiniambia kuwa nimeshinda jambo ambalo lilinishangaza mno na baadae kunifanya kuwa na furaha kubwa.
“Kitaaluma mimi ni Mwalimu hesabu kwenye Shule ya Sekondari Vwawa huko Mbozi, kama unavyojua sisi walimu mambo yetu ya kifedha huwa siyo safi kivilee, ila leo nafuraha sana maana ushindi wangu huu uliotokana na kubeti, umenipa changamoto kubwa.
“Imefika hatua naanza kuamini kuwa hesaba zangu ninazofundisha zipo kwenye damu kwani kama nimeweza kupiga hesabu wakati nabet na leo hii nimekuwa mshindi kati ya watu kibao walioshiriki, nitaendelea kuupenda mchezo huu na kufundisha hesabu zangu kwa wanafunzi kwa kutumia mfano huu,” alisema Mwangasame.
Kwa upande wa Mkurugenzi wa M-BET Dhiresh Kaba yeye amesema kuwa amefurahishwa na ushindi wa Mwangasame, kwani ni mshindi pekee atakayeweza kuutangaza mchezo huu katika mkoa wa Mbeya kwakuwa mara nyingi watu wamekuwa wagumu kuamini kama michezo hii inaendeshwa kwa uwazi na haki.
“Mwangasame kwa sasa namuona kama balozi wetu kwani ndiye mshindi wa kwanza kutokea hapa Mkoani Mbeya na ndiyo maana leo nimeamua kufunga safari kutoka Dar es Salaam kuja kumkabidhi hii fedha ambayo amejishindia baada ya kutumia shilingi elfu moja kubet na leo anaanza maisha mapya kwakupokea zaidi ya shilingi milioni ishirini na nane.
“Kupitia ushindi huu nawaomba Watanzania wote wafahamu kuwa mchezo wa kubet ni wa uwazi na haki, wala hakuna mtu anayeweza kufanya wizi kupitia mchezo huu,Watambue kuwa tunauendesha kwa kufuata taratibu zote za nchi na ndiyo maana leo tumeweza kusafiri na Mkurugenzi wa Michezo ya Kubahatisha Tanzania bwana Tarimba Abbas, ili nae aweze kushuhudia kwa uwazi makabidhiano haya,” alisema Kaba.
Mkurugenzi wa Bodi ya Michezo ya Kubahatisha Tanzania, Tarimba Abbas yeye alitumia muda huo kuwahasa Watanzania na wakazi wa mkoa wa Mbeya kwa ujumla kuwa waendelea kushiriki katika michezo hii ya kubahatisha kwani bodi yao inasimamia kwa ufasaha hivyo haki zote zipo wazi wala hakuna mahali ambapo hawafuatilii hivyo hawezi kukubali mtu akapitisha mwanya wowote wa wizi.
“Mchezo wa kubahatisha ni mchezo uliohalalishwa na Serikali yetu, hivyo nawaomba wakazi wa Mbeya waendelee kuiamini kwakua kila kinachofanyika kipo chini ya mamlaka yetu, ndiyo maana leo nipo Mbeya kwaajili ya kumkabidhi fedha zake Mwangasame, michezo hii ni halali kama ilivyo katika michezo ya soka na mingine yote hapa nchini,” alisema Tarimba.
Habari/Picha: Musa Mateja/GPL.