Mshindi wa M-Bet: Nawapeleka wanangu shule za kimataifa

Mshindi wa kitita cha milioni 126, Willy M. Wadson (katikati) akikabidhiwa mfano wa hudi yake na Meneja Masoko wa M-Bet, Allen Mushi (kulia) huku wakishuhudiwa na Kaimu Msimamizi wa kitengo cha michezo ya kubahatisha wa Mamlaka ya Mapato Tanzania, Mkoa wa Ilala, Philipo Haule.

MSHINDI wa milioni 123 za Perfect 12 ya M-Bet, Willy Wadson ametamba kwamba fedha hiyo aliyoshinda anaenda kuanzisha biashara yake itakayomfanya aendelee kimaisha zaidi na kuwahamishia watoto wangu kwenye shule za kimataifa.

Willy amekuwa mshindi wa tatu wa Perfect 12 ya M-Bet baada ya kubashiri kwa usahihi timu 12 katika mkeka wake. Washindi wengine waliowahi kushinda Perfect 12 ni Frank Kayombo na Simoni Muray.

Mshindi wa kitita cha milioni 126 za M-Bet, Willy M. Wadson akielezea namna alivyofanikiwa kuibuka na kitita hicho.

Mshindi huyo amejishindia kiasi cha milioni 123,614,160 kutoka Kampuni ya Kubashiri Matokeo ya M-Bet.
Akizungumza na waandishi wa habari, Willy amesema atatumia kiasi cha fedha zake kwa ajili ya kuanzisha mtaji, ambao atahakikisha unakua na kuboresha maisha ya familia yake siku zote, pia fedha hizo atazitumia kusomesha watoto wake kwenye shule za kimataifa.

“Kwangu binafsi nimefurahi sana kuwa mshindi wa Perfect 12 ya M-Bet, nimekuwa nikicheza huu sasa mwaka wa tatu na kila siku natumia kiasi cha elfu 5000 ama zaidi. Nimeshahinda huko nyuma lakini siyo kiasi kikubwa kama hiki.

Willy M. Wadson akiwa ameshikili hudi yake.

“Mimi ni mkulima pia nafanya kazi ya kubadilisha fedha, hizi fedha nilizoshinda nitazitumia kwa ajili ya kuboresha biashara zangu na pia nitaangalia uwezekano wa kuwahamishia watoto wangu katika shule za kimataifa.
“Niwaambie Watanzania kwamba hizi fedha za ushindi kutoka M-Bet ni za kweli na ukishinda unapewa chako, hakuna suala la upendeleo hata kidogo,” alisema Willy ambaye ni shabiki wa Simba na Manchester United.

 

Meneja Masoko wa M-Bet, Allen Mushi yeye amekazia kwa kusema: “Nilisema sisi M-Bet tukianza kuzimwaga tunazimwaga kweli, huyu ni mshindi wa tatu sasa wa Perfect 12 na zaidi ya milioni 500 zimetoka, kwetu dau linaongezeka kila siku pale inapotokea hatujampata mshindi.

“M-Bet ni walipaji kodi wazuri na katika kila mshindi anayepatikana basi hapo tunalipa kodi, kwa huyu Willy kuna kodi ya milioni 24 ambayo serikali inapata hivyo yeye atabakiwa na kiasi cha milioni 98,” alisema Allen.

 

Toa comment