The House of Favourite Newspapers

Mshindi wa Nyumba na Milioni 20 Mbeya Akabidhiwa Fedha Zake

Mshindi wa pili wa nyumba na sh Milioni 20 wa bahati nasibu ya Biko, Alex Nyoka, amekabidhiwa fedha zake leo mjini Mbeya, ikiwa ni siku moja baada ya kuibuka kidedea kutoka kwenye droo ya 158 ya Biko.
Makabidhiano hayo yamefanyika leo Lujewa, Mbalari mkoani Mbeya, akiwa mtu wa pili mwenye bahati aliyeshinda nyumba ya kisasa na fedha kutoka Biko, akitanguliwa na Prisca Msuya, aliyeibuka kidedea siku kadhaa zilizopita.
Akizungumza katika makabidhiano hayo, Nyoka ambaye ni dreva wa tax, aliishukuru Biko kwa kumkabidhi fedha zake sh Milioni 20 mapema, huku akiisubiri kwa hamu nyumba yake kutoka Biko.

Zawadi za papo kwa hapo za Biko kuanzia sh 5,000, 10,000, 20,000 hadi sh Milioni moja zinaendelea kutolewa kwa kupitia Biko inayochezwa kwa kufanya miamala kwenye simu za mikononi ya Tigo Pesa, Mpesa na Airtel Money kuanzia sh 1,000 na kuendelea, namba yao ya Kampuni ni 505050 na ile ya kumbukumbu ni 2456.

 

Droo kubwa huchezeshwa kila Jumatano na Jumapili, huku kuanzia Jumatano na Jumapili,  watanzania wanaocheza Biko wakitarajiwa kushinda nyumba na sh Milioni 20.

Na Mwandishi Wetu, Mbeya

Comments are closed.