Mshindi wa Shilingi 500,000 wa Maokoto ya Serengeti Akabidhiwa Zawadi Yake Kilosa
Washindi mbalimbali wanaendelea kujishindia maokoto kupitia vizibo, zoezi linaloendeshwa na Kampuni ya Serengeti Breweries.
Awamu hii ni zamu ya Martha Manywa, Mkazi wa Kilosa mkoani Morogoro ambaye amejishindia kiasi cha shilingi 500,000 taslimu.
Martha amekabidhiwa zawadi hiyo na Mwakilishi wa Mauzo wa Serengeti Breweries, Shomari Mohammed, hafla iliyofanyika katika Baa ya Comer Pub iliyopo Dumila Wilayani Kilosa Mkoani Morogoro jana Ijumaa.