MSHTUKO MCHUMBA WA JUX, ADAIWA KUFANYA UPASUAJI MARA 6

DAR ES SALAAM: ACHANA na bata analokula akiwa na staa wa muziki wa RnB Bongo, Juma Khalid ‘Jux’ mara wapo kwenye Viwanja vya Mlimani City mara Hifadhi ya Wanyama Serengeti mkoani Mara! Habari mpya ikufikie kuwa mrembo anayedaiwa kuwa ni mali halali ya msanii huyo, Nayika Thongom, ameleta mshtuko wa ajabu.  Nayika anadaiwa kufanyiwa upasuaji mara sita ili kutengeneza shepu aliyo nayo kwa sasa. Nayika ambaye ni nesi na miongoni mwa wanamitindo maarufu nchini kwao, Thailand anadaiwa kufanyiwa upasuaji sehemu mbalimbali za mwili wake ambao umemletea muonekano alionao sasa.

Kwa mujibu wa vyanzo kutoka Thailand, vimeanika picha pamoja na hatua za operesheni hizo sita kuanzia kwenye sura yake, chini ya kidevu, matiti, kiuno, mapaja, eneo la katikati ya mapaja pamoja na pua.

Mara baada ya kufanyia operesheni hizo sita, Nayika ambaye amesomea mambo ya madawa nchini China alisema licha ya mama yake mwenye asili kutoka Misri kuwa na umbo zuri, alikuwa na ndoto ya kuwa na muonekano tofauti baada ya kusemwa sana tangu akiwa mdogo kuwa hana umbo la kuvutia, jambo lililomnyima uhuru wa kujitokeza mbele za watu.

“Mwanzoni nilikuwa mnene sana na mwenye ngozi nyeusi kiasi cha kuitwa nguruwe. Nilishaachwa na mwanaume, kisa aliniambia mimi ni mbaya. “Ilikuwa ngumu kupata mwili sahihi na kuwa kama nilivyo. Nimetumia gharama kubwa sana kuwa hivi. “Nakumbuka nilishauriana na daktari wangu na kufikia uamuzi wa kufanya operesheni hizi sita kwa sababu nilitaka kuwa na mwili mzuri na wa kuvutia.

“Wakati mwingine unatakiwa ukubali kuwa mazoezi hayawezi kukupa kila kitu unachokitaka katika mwili wako,” alisema Nayika ambaye makazi yake kwa sasa yapo katika Jiji la Shenzhen nchini China. Nayika na Jux uhusiano wao ulianza kujulikana mara baada ya kuonekana pamoja wakijiachia kimahaba

ndani ya Hifadhi ya Wanyama ya Serengeti. Siku chache mbele walionekana tena pamoja katika Viwanja wa Mlimani City kwenye sherehe ya kuzaliwa ya mama wa staa wa Bongo Fleva, Nasibu Abdul ‘Diamond Platnumz’, Sandra Kassim ‘Sanura’ na Tanasha Donna Oketch.

Wawili hao kwa sasa ni habari ya mjini kutokana na kujiweka kistaa katika mitandao ya kijamii wakila bata katika viunga mbalimbali vya starehe Dar na visiwani Zanzibar. Kabla ya kudaiwa kuwa na Nayika, Jux alikuwa katika uhusiano wa kimapenzi na msanii mwenzake, Vanessa Mdee ‘Vee Money’ ambao uhusiano wao ulienda mbali zaidi kwa kufanya kazi nyingi za pamoja ikiwa na kuandaa tamasha la pamoja na In Love & Money ambalo walizunguka pamoja ndani na nje ya nchi.

 


Loading...

Toa comment