The House of Favourite Newspapers

MSHTUKO: UTAJIRI WA GHAFLA WA MSANII BONGO MUVI WASHTUA!

MSANII wa Bongo Muvi wa ‘long time’, Gladys Chiduo ‘MC Zipompa’ ambaye hivi karibuni amebadili jina na kutaka aitwe Madam amewashtua watu baada ya kubainika kuwa, sasa hivi ametembelewa na utajiri wa ghafla bila kujulikana chanzo ni nini.  

 

Staa huyo ambaye pia anafanya vizuri kwenye kazi ya U-Mc awali alikuwa akiishi Sinza Mapambano jijini Dar kwenye chumba na sebule lakini siku za hivi karibuni zilivuja taarifa kuwa, anaishi kwenye mjengo wa kifahari uliopo Bunju jijini Dar huku akimiliki magari manne.

 

MADAI YA UTAJIRI

Rafiki wa karibu wa Zipompa aliyeomba hifadhi ya jina lake alilitonya Risasi Mchanganyiko kuwa, mwanamama huyo amekuwa akibadili magari kila siku na kwamba anaishi kwenye nyumba ya ghorofa, jambo linalowafanya watu wajiulize mafanikio hayo ya harakaharaka kayapataje.

“Nyie mnasema hali ni ngumu, hivi mnajua kuwa Zipompa ana maisha mazuri ya ghafla tu, sijui amempata bwana gani anayemuweka mjini kwani anakaa kwenye ghorofa kubwa ambalo nyuma lina ghorofa nyingine ndogo, amemuweka mama yake humo. Yaani ukimuona si mwenzako kabisa, hata usafiri anaotumia ni wa kishua, anabadili magari kila kukicha,” alifunguka sosi huyo.

 

Baada kupatikana kwa madai hayo kisha waandishi wetu kuelekezwa ulipo mjengo wa msanii huyo, walifunga safari hadi eneo liitwalo Bunju-Masaiti ili kupata ukweli wa mambo. Baada ya kufika eneo hilo na kuuona mjengo huo ambao katika mazingira ya kawaida ni vigumu kuamini kama mwanamama huyo ndiye anayemiliki, waandishi hao walipiga hodi na mlinzi alitoka kisha kufungua geti.

Risasi: Habari yako kaka.

Mlinzi: Salama tu, niwasaidie nini?

Risasi: Samahani, hapa ni kwa Zipompa?

Mlinzi: Hapana, hapa ni kwa Madam.

Risasi: Ndo’ huyohuyo.

Mlinzi: Nimwambie nyie ni nani?

Risasi: Mwambie waandishi wa Global.

Mlinzi huyo aliondoka kisha baada ya dakika mbili alirejea na kuwakaribisha ndani waandishi ambao walikutana uso kwa uso na Zipompa aliyekuwa na uso uliojawa na tabasamu.

Zipompa: Karibuni, naona mmenivamia.

Risasi: Asante, tumeona tuje bila taarifa maana habari tulizopata zilitushtua kidogo, tukaona leo lazima tukupate tujue ukweli.

Zipompa: Mhh! Na nyie kwa kufuatilia mambo ya watu, enhe, hebu niambieni lililowaleta maana mmenitisha.

Risasi: Kwanza hongera sana, tumesikia hapa tulipo ni kwako, maisha yamekubadilikia ghafla, nini siri ya haya mafanikio, nani kakuhonga?

Zipompa: Ni kweli kabisa hapa ni kwangu, yaani kwangu kabisa na niwaambie tu kwamba, wala sijahongwa. Nyumba hii amenizawadia mwanangu anaitwa Kheri.

 

Risasi: Mwanao ndo’ kakupa hii nyumba? Kwani wewe una mtoto mkubwa anayeweza kumiliki nyumba ya kifahari kama hii na mbona hatujawahi kumuona?

 

Zipompa: Hahaha! Siyo kwamba nina mtoto mmoja, ninao watatu, wawili wa kiume na mmoja wa kike, wote wanaishi nje ya nchi, nashukuru Mungu kwa hilo.

Risasi: Mbona kuna madai kuwa umepangishiwa na ‘danga’ flani hivi?

Zipompa: Hakuna ukweli wowote, mimi naheshimika kwa sababu ya wanangu. Kwanza danga gani la kunipa jeuri hii niliyonayo? Hii ni faida ya kuzaa.

 

Rasasi: Sasa huyu mwanao kainunua, kakujengea au imekuwaje mpaka ikakufikia wewe?

Zipompa: Mwanaume niliyezaa naye ambaye ni marehemu alikuwa na mali nyingi, baada ya mirathi kugawanywa, mwanangu alipewa hii nyumba na ndipo aliponipa mimi kwa kuwa yeye anaishi nje.

 

Risasi: Hivi hii nyumba inaweza kuwa na thamani ya shilingi ngapi?

Zipompa: Ni takribani milioni mia tano.

Risasi: Tumeona hapo nje kuna magari kama yote, nayo ni yako?

Zipompa: Swali hilo pigia mstari tu, ni magari yangu yote manne. Tata Safari VX, Mercedes Benz C 200, Toyota Prado na Toyota Hiace.

Risasi: Unajisikiaje kutoka kwenye chumba kimoja na sebule hadi kumiliki mjengo huu wenye hadhi ya kitajiri?

 

Zipompa: Ukweli namshukuru Mungu, naamini yupo, anaweza asikupe leo akakupa kesho.

Baada ya mahojiano hayo, waandishi wetu walipata fursa ya kushuhudia sehemu mbalimbali za nyumba hiyo na kuthibitisha kuwa, ni kati ya nyumba za kitajiri zilizopo kwenye Jiji la Dar na msanii huyo hakika ameyapatia maisha.

GIGY MONEY; Mimi ni mzuri wanaume wanapagawa/ Cardi b ameniiga

Comments are closed.