The House of Favourite Newspapers

MSIBA HAUNA VIGELEGELE

YAANI shoga yangu leo nimekaa zaidi ya nusu saa natafa­kari meseji moja tu! Hata kama wa­nawake tumeum­biwa mateso si kwa aina hii kwa kweli, loooo!  

 

Ngachoka! Kama wasemavyo Wacha­ga! Shoga hili la leo siyo kunifika hapa tu bali limenifika huku! Kuna wanaume wana roho za kikatili sijawahi kuona. Yupo radhi afurahie na mchepuko la­kini kwako uambulie maumivu!

 

Leo acha niwape vidonge vyenu mkinuna litakuwa limewaingia lakini yangu ya moyoni nimeyatapika, au naongopa shoga yangu? Hatukatai sisi wanawake wakati mwingine akili zetu tunakuwa kama vile tumebebewa na kushindwa kutam­bua nje ya boksi!

 

Nasema yote hayo kwa sababu shoga! Nimeamua kuanza kwa kusema msiba hauna vigelegele ili uelewe ni msiba gani huo! Kuna msomaji amenitumia meseji ya malalamiko ya familia yake, itakuwa vizuri kama nikiianika meseji yake ili nawe upate cha kujifunza; “Shoga mimi ni mama wa watoto wawili japokuwa nai­shi na watoto watatu. Mtoto wangu wa tatu shoga ametoka kwa mama mwingine.

 

“Kilichonifanya nije hapa shoga ni tabia ambayo kama mwan­amke nafanyiwa kila siku, mume wangu alipokuwa akitaka kunioa hakuniweka wazi kama ana mtoto wa nje, nikamkubalia taratibu zikafanyika na kuolewa. Baada ya kupita miaka sita nikiwa nimezalishwa watoto wawili, kuna mwanamke alikuja kumbwaga mtoto wa miaka minne na kusema amezaa na mume wangu.

“Niliumia sana kwa kweli baada ya kum­bana mume wangu akakiri, nilijishusha na kuanza kumlea mtoto huyo sawa na wanangu wa kuwazaa, nilimpenda sana. “Ili kufupisha maelezo shoga, sasa hivi mume wangu ameku­wa hashau­riki, amer­udisha uhu­siano na yule mwa­namke ali­ye­zaa naye, kila nikim­wambia anaku­wa mkali na wakati mwingine anani­piga sana.

 

Amenipi­ga maru­fuku kumse­mea hata kwa wazazi wan­gu wala wake. “Shoga naom­ba nisaidie ushauri, naogopa asije akapata mtoto mwingine kisha aje anibwagie.”

 

Niwageukie nyie wanawake wenzangu, kuna kipindi sawa unakuwa na huruma lakini unaangalia na maisha yako! Mwanaume kama huyo anakuz­iba mdomo usifike kwa wazazi wako wala wake kisha yeye anaendelea kuku­fanyia hivyo unasubiri miujiza gani kama siyo kuwa punda wa jang­wani?

 

Hii imekuwa tabia kwa wa­naume wengi siyo kwako tu, wakipata mke wa kumuoa huyo­huyo wanamrundikia watoto wa nje na mbaya zaidi wanashindwa kuwalea vizuri kwa kutegemea mke aliyenaye ndiyo kila kitu. Yaani wamekuwa wakiwachuku­lia wake zao kama gari bovu vile, wanaliegeshea kwenye mterem­ko liserereke lenyewe!

Shoga nimeumia! Nimeumia! Nimeumia! Nimetamani sana nikutane na huyo mwanaume nimpe mfano wa wanawake tu­livyo kama Anti Nasra hajaita Anti Ng’aa! Na sisi wanawake jamani, mwanamke unatakiwa kuwa na maamuzi yako inapofikia hatua kama hii ndiyo maana matukio kama haya naona kama msiba kwa nini kupigwe vigelegele!

 

Sawa mwanaume ana haki ya ku­kutawala lakini siyo kwa kupitiliza kiasi hiki, shuuuutuuuuuu! Kwa leo naomba niishie hapa maana si kwa kuniharibia siku yangu. Ni mimi Anti Nasra Shang­ingi Mstaafu.

Comments are closed.