Msiba wa Filikunjombe, wengi wazimia Ludewa

DSC_1132

Mke wa Filikunjombe akilia kwa uchungu.

Gabriel Ng’osha

Chema hakidumu! Vilio na majonzi vimelitawala Jimbo la Ludewa na nchi nzima kwa jumla, huku mamia ya wakazi wa jimbo hilo lililokuwa likiongozwa na mchapakazi, marehemu Deo Filikunjombe aliyeaga dunia Alhamisi iliyopita kwa ajali ya helkopta iliyotokea katika Hifadhi ya Selous eneo la Msolwa mkoani Morogoro, wamezimia kutokana na mapenzi ya dhati waliyokuwa nayo kwa shujaa wao huyo.

DSC_1133

….Akifarijiwa.

Baada ya kuagwa katika Hospitali ya Jeshi ya Lugalo, nyumbani kwake Kijichi jijini Dar kisha kusafirishwa kwenda nyumbani kwao Ludewa mjini, vilio vilitawala jimboni humo.

Mamia ya wakazi wa jimbo hilo walio wengi walijikuta wakizimia tangu walipopata taarifa ya msiba huo na mwili ulipowasili nyumbani kwao.

“Mwanangu Filikunjombe, umeondoka ukiwa bado tunakuhitaji, wewe ulikuwa mtetezi wa mamalishe, watoto na wasiojiweza, tutakimbilia wapi sisi jamani baba Deo,” alisikika mama mmoja mtu mzima akilia kwa uchungu nyumbani kwa Filikunjombe, Kijichi.

DSC_1130

Waombolezaji wakiwa msibani.

Mmoja wa viongozi wa chama cha upinzani alisikika akisema: “Hakuna atakayebisha kuwa Filikunjombe alikuwa mchapakazi.

Kama yupo atakuwa muongo na mnafiki kwani tulishirikiana naye katika kazi mbalimbali iwe shamba, kuchimba mitaro, kuvuna mazao, magengeni, kwa jumla katika suala la maendeleo ya jimbo hakuwa na uchama.

Naye mmoja wa vijana kutoka jimboni humo, Elly Bonke alisema: “Tumepoteza mtu muhimu sana, nguvu kazi ya jimbo na taifa, mshauri na mkombozi wetu vijana, alipenda tuchape kazi, alikuwa tayari kushirikiana nasi katika maendeleo yetu kwa kutupatia mashine za kurahisisha kazi mbalimbali kama vile compressor, majenereta na kadhalika.’’

DSC_1143Marehemu Filikunjombe ameacha simanzi kubwa kwa chama chake cha CCM na hata kwa vyama vile vya upinzani kutokana na uchapakazi wake.

Loading...

Toa comment