The House of Favourite Newspapers

Msichana aeleza anavyowamaliza wanaume wakware!

0

msichana

Mayasa Mariwata na Gladness Mallya
Ama kweli dunia imekwisha! Msichana aliyejitambulisha kwa jina la Grace, mzaliwa wa mkoani Njombe ameibuka na kusimulia jinsi ambavyo anajiachia kimapenzi na idadi kubwa ya wanaume kwa siku, eti kwa kuwa ni dhambi kwake kumkataa mwanaume, jambo lililosababisha amkimbie mumewe aliyemtaja kwa jina la Veris, mkazi wa Kipawa jijini Dar.

Akizungumza kwenye mahojiano maalum juzikati ndani ya chumba cha habari cha gazeti hili huku akirekodiwa, Grace ambaye ana kila sifa ya kuwavutia wanaume alisimulia kwamba, anachokifanya ni kujikita kwenye maovu kwa kufanya ufuska wa kila namna huku akipita maeneo mbalimbali kuwahamasisha watu kufuata nyayo zake.

“Nimesoma na nina ujuzi kwenye mambo ya ustawi wa jamii, lakini kabla ya kumaliza chuo, nilizaa watoto watatu na wanaume tofauti ndipo nikaolewa na kuamua kuachana na mume wangu mwezi mmoja uliopita na kuamua kujiachia tu.

“Ukikaa baa, ukalewa au ukiwa gesti unavunja amri ya sita basi uko pamoja na mimi, naamini hakuna mwanamke mwenye idadi kubwa ya kutembea na wanaume wengi kama mimi.

“Ndugu zangu huwa wanajua nina matatizo ya akili lakini nilipopimwa hospitali nilikutwa nipo sawa.

“Yaani kwa siku nzima huenda wakafika hata zaidi ya wanaume thelathini ninaokutana nao kimwili. Wengine wananipa fedha na wengine hawanipi,” alisema msichana huyo kwa macho makavu bila tone la aibu.

Akiendelea kuzungumzia jinsi alivyokithiri kwenye uasi wa dunia, Grace alitiririka kwamba, kuna siku anakutana na wanaume ambao hawana fedha ya kumpa hivyo ili asilale njaa usiku huwa anaenda kujiuza barabarani kama wafanyavyo machangudoa na kujikuta ametembea na idadi kubwa ya wanaume bila kujali pato analoingiza wala thamani ya mwili wake

Leave A Reply