Msemaji Mkuu wa Serikali: Tutaanza Kuuza Umeme Nje ya Nchi, ‘Kasongo’ hayuko hatarini kutoweka – Video

Katibu Mkuu wa Wizara ya Habari, Utamaduni, Sanaa na Michezo, na Msemaji Mkuu wa Serikali, Gerson Msigwa, leo Januari 25, 2025 amesema kuwa Tanzania inazalisha umeme megawati 3,410 zaidi ya mahitaji ya kawaida ikilinganishwa na matumizi ya megawati 1,888 ambapo kwa sasa wameanza kujenga miundombinu ili kusafirisha umeme kutoka bwawa la Mwalimu Nyerere kwenda nchi ya Kenya na Zambia.

Msigwa, amesema mnyama ngiri maarufu kwa jina la “kasongo” hayuko hatarini kutoweka kutokana na wingi wa wanyama hao katika hifadhi za wanyamapori.
Kasongo ameendelea kujizolea umaarufu, hasa katika mitandao ya kijamii, kutokana na mwendo wake wa kipekee na tabia ya kuonesha dharau anapofukuzwa na wanyama kali msituni bila kusahau kasi yake.
Msigwa ameyasema hayo wakati akizungumza na waandishi wa habari katika Hifadhi ya Mikumi na kuongeza kuwa serikali inaendelea kuimarisha miundombinu ya kusambaza umeme ndani ya nchi ili kuondoa kukatika umeme.