The House of Favourite Newspapers

Msikie Carlinhos Kuhusu Nafasi yake Yanga

0

KIUNGO mshambuliaji wa Yanga, Carlos Fernandes ‘Carlinhos’, amefunguka kwamba hivi sasa tayari ameshapona majeraha yaliyokuwa yakimsumbua na kutoonekana kwake uwanjani kunatokana na maamuzi ya benchi la ufundi.

 

Carlinhos aliyejiunga na Yanga mwa msimu huu, amekuwa akipitia kipindi kigumu cha majeraha ambayo yamemfanya kuwa nje ya uwanja tangu Novemba mwaka jana.

 

Nyota huyo alianza vizuri msimu huu akihusika kwenye mabao manne ya Yanga, akifunga mawili na kuasisti mara mbili, lakini kwa sasa hasikiki kutokana na kutocheza kwa muda mrefu.

 

Akizungumza na Spoti Xtra, Carlinhos alisema: “Ni kweli hapo nyuma nilikuwa na majeraha ambayo yaliniweka nje ya uwanja kwa muda mrefu, lakini tayari nimeshapona na kwa sasa nipo sawa kwa ajili ya kuisaidia timu yangu kupata matokeo mazuri uwanjani na kuweza kufikia malengo yetu.“Kuhusiana na ishu ya kutocheza, hilo suala lipo kwenye uamuzi wa benchi la ufundi.”

STORI: JOEL THOMAS

Leave A Reply