LIGI Kuu Bara msimu uli-opita wa 2016/17 umefikia tamati juzi Jumamosi, mambo mengi yamepita lakini mengi yake yakiwa ni mafunzo kwa timu husika hasa mambo ya kiutendaji.
Ulikuwa msimu ambao kila timu ilionekana kuwa na hamu ya kufanya vizuri hata klabu ambazo zilizoeleka kutofanya vizuri, safari hii zilikomaa na kufanya vi-zuri.
Kuna wakati Simba iliongoza ligi kwa tofauti ya pointi nane na Yanga iliyokuwa nafasi ya pili, ni kama wanaoongoza walijisahau na kujiona wameshamaliza kazi, Yanga ikaja ikawapita.
Hiyo ina maana kwamba, Simba iliona imeshamaliza kazi wakati huo kumbe ilitakiwa kupambana ku-hakikisha haipotezi kirahisi mechi zake. Pia Yanga ilionyesha hali ya kupambana na kutokata tamaa mapema.
Kuna klabu zilianza kwa kulegalega labda zikitegem-ea kufanya vizuri baadaye, hizo hazikujua biashara ni asubuhi na jioni ni mahe-sabu. 2016/17 ulikuwa ni msimu wenye somo kubwa kwetu, klabu zitumie haya yaliyojitokeza ili kuwa ima-ra msimu ujao.