The House of Favourite Newspapers

Msiniletee Sapraiz Za Kijinga!

0

vegeterians-couple-bedHaya mambo ya kuiga haya yatatupeleka pabaya. Halafu kiukweli mi nazilaumu sana TV zinatuonesha mambo mengi na sisi tunaiga hapo hapo bila kutafakari, kwa kuwa tu Mzungu kayafanya.

Na siku hizi kwa kuwa tuna masupastaa basi wao ndiyo huwa wa kwanza kuiga mambo mengi kisha wengine tunafuatia. Siku hizi kila mdada anataka kuwa na nywele za kizungu, kipilipili kimeuawa, wamebaki nacho wakaka wachache, maana kuna wengine nao usishangae ukiwaona na nywele zinateleza kama za Mzungu.

Wadada wenye asili ya kipilipili siku hizi wana nywele ndefu tena za rangi mbalimbali, nyingine za rangi ya dhahabu, nyingine za bluu, kijani basi ni vuluvulu tupu. Halafu hii inasumbua sana kiutamaduni, zamani waganga waliweza kukuagiza upeleke unywele wa mpenzi wako ili atulie kwako, siku hizi ukipeleka unywele unajisumbua maana unapeleka unywele wa kutoka China.

Mganga anaishia kumroga Mchina. Nikumbushe tu kuna methali inasema akili ni nywele kila mtu ana zake, sasa unapovaa nywele za mtu mwingine kama alikuwa fala na wewe ujue ndiyo  hivyohivyo.

Muwe mnaulizia historia ya mtu ambaye umevaa nywele zake, unaweza kuanza kufanya ujingaujinga ghafla kumbe sababu ya nywele.

Balaa lingine la kuiga ni hili la siku hizi mpaka vijijini wanaume wazima wanatembea wameshusha suruali ili bukta za ndani zionekane, bila kujali ni safi au la, masupastaa wametuletea balaa hili la wanaume kuanza kufanana na nyani kwa kukosa mavazi sehemu ya kukalia.

Lakini yote tisa kumi ni hiki kitendo cha kusherehekea siku ya kuzaliwa kwa kumwagiwa maji au pombe. Halafu mbaya zaidi eti ni sapraizi! Mtu umetoka zako mahala huna hili wala lile unaingia kwenye chumba ghafla unamwagiwa pombe, hivi hizi ni akili kweli au ufala unaotokana na kuvaa nywele za Mchina mmoja aliyekuwa fala kwao?

Sasa natoa onyo siku yangu ya kuzaliwa inakuja atakayekosea na kunilowesha ajue kwanza tunaanza ngumi hapohapo halafu mahakamani anaenda huku ana manundu kibao.

Leave A Reply