The House of Favourite Newspapers

Msomi UDSM Aibuka Miss Dar Indian Ocean

0
Washiriki wa Miss Dar Indian Ocean  wakijinadi.

 

Msomi wa Chuo Kikuu cha Ardhi kilichopo Mlimani jijini Dar, Stellah Ernest, usiku wa kuamkia leo ameibuka mshindi wa taji la Miss Dar Indian Ocean katika kinyang’anyiro kilichofanyika Ukumbi wa New Msasani Club jijini Dar.

 

Miss Dar Indian Ocean aliyemaliza muda wake (aliyekaa) akiwagaa watamaji.

 

Stellah alivishwa taji hilo baada ya kuwabwaga wenzake 15 katika mavazi ya ubunifu, jioni na ufukweni. Sambamba na mavazi alionesha umahiri wa kujieleza kwa ufasaha na kuonesha upeo mkubwa alionao.

 

Mshindi wa taji hilo, Stellah Ernest (katikati) akiwa na washiriki wengine waliongia tano bora.

 

Akizungumza na baada ya mshindi huyo kutangazwa, Mkurugenzi wa Grace Entertainment, Catherine Ambakisye ‘Mama Rolaa’ alisema mshindi huyo alikuwa na haki ya kutwaa taji hilo kutokana na vigenzo mbalimbali alivyowazidi wenzake siku zote walipokuwa kambini.

 

Washiriki wote wakiwa na mshindi.

 

Mama Rolaa alimalizia kwa kuushukuru Uongozi wa Global Publishers kwa kujitolea kudhamini mashindano hayo kupitia Magazeti yake ya Uwazi , Ijumaa, Amani, Risasi, Ijumaa Wikienda, Championi na Global TV Online.

Washiriki wote wakiwa na mshindi.

 

Mshindi akiwasalimia watazamaji.

 

Mshindi akikabidhiwa taji na Isabella Mpanda (Bella).

 

Majaji wakijadiriana.

STORI/PICHA: RICHARD BUKOS NA ISSA MNALLY.

Leave A Reply