Msondo Music Band Walivyokiwasha Kisuma Usiku wa Kuamkia Leo

BENDI ya Msondo Music, usiku wa kuamkia leo imekiwasha ile mbaya ndani ya Ukumbi wa Kisuma uliopo Mbagala Sabasaba Dar.

Kama ilivyo kawaida ya bendi hiyo kukusanya umati mkubwa wa mashabiki ndivyo ilivyokuwa kwenye onesho hilo ambapo makamuzi yalikuwa si mchezo.

Mpiga solo gitaa wa bendi hiyo, Ridhiwani Pangamawe aliyeachiwa gitaa hilo na marehemu Mzee Said Mabera waliyekuwa wakipokezana aliwachagiza mashabiki hao ile balaa.

Mashabiki baada ya kupandwa mizuka walivamia steji na kuanza kubanjuka kwa raha zao.            Angalia picha mambo yalivyokuwa.

Mpiga Solo, Ridhiwani Pangamawe akicharaza nyuzi kwa hisia kali.

Hassan Moshi TX Junior kazini

Shabiki raha kama zote.

Mambo ya kuserebuka.

                                                        Athumani Kambi akipelekeshana mdogomdogo na shabiki.                                                                 

Mpiga besi gitaa Davido Besi akiwajibika.

        Waimbaji wa Msondo katika shoo hiyo kutoka kushoto Athumani Kambi, Edo Sanga na Juma Katundu.            HABARI/PICHA ZOTE NA RICHARD BUKOS /GPL 

Toa comment