Msondo Wafunika Leaders Club
Waimbaji wa Msondo Ngoma wakionesha ujanja wao kwa mashabiki.
BENDI kongwe ya muziki wa dansi nchini, Msondo Ngoma jana ilifunika vilivyo katika tamasha kubwa la kumuunga mkono Mkuu wa Mkoa wa Dar es Salaam, Paul Makonda katika kampeni ya kuchangia madawati mashuleni.
Tamasha hilo lilifanyika jana usiku katika viwanja vya Leaders Club, Kinondoni jijini Dar ambapo sehemu ya mapato ya tamasha hilo yatatumika kununulia madawati.
Akizungumza katika hafla hiyo, Makonda alisema serikali itaendelea kutoa sapoti kubwa kwa wanamuziki wa dansi ili kuuendeleza na kuuboresha muziki huo ili ufike mbali kama ilivyokuwa siku za nyuma.
Miongoni mwa bendi zilizotoa burudani kwenye tamasha hilo ni Msondo Ngoma, Mlimani Park, Yamoto, QS International na nyingine nyingi.
Msondo Ngoma wakitoa burudani.
Wapiga gitaa wa Msondo Ngoma katika ubora wao.
Mlimani Park wakitoa burudani.
Mlimani wakiendelea kutoa burudani.
Mwimbaji wa bendi ya QS International akiimba kwa hisia kali.
QS wakiendeleza makamuzi.
Mpiga ngoma wa Msondo Ngoma akionesha utundu wake.
Msondo wakiendelea kutoa burudani.
Wanamuziki wa Ya Moto Bendi wakitoa burudani.
Ya Moto Bendi wakiendelea kutoa burudani.
Ya Moto Bendi ikizidi kuwaburudisha mashabiki.
Mkuu wa Mkoa wa Dar, Paul Makonda akizungumza jambo mbele ya wanamuziki hao (hawapo pichani).
NA DENIS MTIMA/GPL