Mstaafu Kikwete Awapongeza Wanawake Kuongoza Uhitimu UDSM
Dar es Salaam: 30 Novemba 2024: Rais Mstaafu wa awamu ya nne na Mkuu wa Chuo Kikuu cha Dar es Salaam (UDSM) Jakaya Mrisho Kikwete, leo amehutubia wakati wa Mahafali ya 54 duru ya nne ya 2024, na kusema kuwa amefurahi kwamba msimu huu wanawake ni wengi kuliko wanaume na hilo ndilo jambo kubwa la mafanikio katika chuo hicho na kwa Taifa kwa ujumla.
Kikwete amesema na kuongeza kwa kusema kuwa kuwa mafanikio hayo yamepatikana kwenye elimu ya msingi usawa wa jinsia na kwenye elimu ya sekondari ambapo changamoto kubwa ilikuwa kwenye elimu ya juu na hasa kwenye vyuo vikuu.
“Tumekwenda tumefika hapa tulipo ni mafanikio makubwa sana inastahili pongezi Serikali na wananchi wa Tanzania kwa hapa tulipofikia inafika mahali inatufukirisha hivi hawa watoto wa kiume wako wapi?
Wanakwenda wanaanza kuonekana wanapungua lakini siyo kwamba nasikitika kama mwanaume kwa kilio cha kuona kwamba wanawake miaka yote mingi walikuwa wanaonekana kuwa wako nyuma lakini sasa wako mbele na wanawake kuwa mbele sasa wanaume nao wajitahidi ili kuwe na ushindani.” Alimaliza kusema Kikwete.