The House of Favourite Newspapers

‘Msukule’ nyumbani kwa tajiri aibua mazito

0

Msukule (4)-001Juhudi za kumtoa shimoni zikiendelea.

Mayasa mariwata, AMANI
DAR ES SALAAM: YULE mwanadada aliyekutwa kwenye shimo la majitaka ambalo halijaanza kutumika nyumbani kwa mfanyabiashara aliyejulikana kwa jina moja la Mtei na kudhaniwa na watu kuwa labda ni msukule, Upa ameibua mazito.

Kwa mujibu wa chanzo kutoka Jeshi la Polisi Kinondoni, mdada huyo ametoweka katika mazingira ya kutatanisha akiwa kwenye Kituo cha Polisi Mbezi jijini Dar tayari kwa kumpeleka hospitali.

“Jamani mna habari yule dada aliyekutwa shimoni mwa mfanyabaioshara Mtei kule Kibamba, amepotea katika mazingira ya kutatanisha? Nimewaambia nyie maana nimeona leo (juzi Jumanne), mmeandika kwenye Gazeti la Uwazi,” alisema afande mmoja.

Gazeti hili lilianza kufuatilia undani wa habari hiyo ambapo, vyanzo vya uhakika vinasema kuwa, ni kweli mwanamke huyo (mwenye watoto wawili) alitoweka kimaajabu.

msukulee-001Baada ya kutolewa shimoni.

Akizungumza na kituo kimoja cha redio cha jijini Dar, Jumatatu iliyopita, Kamanda wa Polisi Mkoa wa Kinondoni, ACP Christopher Fuime alisema ni kweli mwanadada huyo alitoweka kituo cha polisi.

Habari za awali zilizolifikia gazeti hili Jumatatu iliyopita zilisema kuwa, baada ya polisi kumtoa kwenye shimo walimpeleka Hospitali ya Rufaa ya Tumbi, Kibaha, Pwani.
Siku hiyohiyo, mapaparazi wetu walifika Tumbi na kukutana na Afisa Uhusiano wa Hospitali ya Tumbi, Rose Didas ambaye alisema hana taarifa za kupokelewa kwa mtu huyo hospitalini hapo.

“Mtu huyo hapa hayupo na angekuwepo ningejua. Labda amepelekwa Hospitali ya Mwananyamala,” alisema Rose.

Jumatatu iliyopita, Amani lilimtafuta askari mmoja wa Kituo cha Mbezi ambaye alisema anavyojua yeye, mwanamke huyo alipelekwa Tumbi.

Juzi Jumanne, baada ya maelezo ya Afande Fuime, gazeti hili lilimpigia simu askari mmoja wa Kituo cha Mbezi na kumuuliza ambapo alisema kuwa, bosi wake (wa kituo cha Mbezi yu njiani kwenda Tumbi).

“Mpigie bosi wangu… (akamtaja jina), yeye anakwenda Tumbi kuangalia hali yake,” alisema afande huyo akiomba hifadhi ya jina lake.

Amani likampigia simu bosi huyo na kumuulizia kuhusu maendeleo ya Upa.
“Kwa sasa niko kwenye kikao kwa RPC (Fuime), hebu piga baadaye,” alisema bosi huyo.

Wakizungumza na kituo kimoja cha redio cha jijini Dar, watu waliojitaja kuwa ni ndugu wa mwanamke huyo ambaye ni mkazi wa Buruguni Rozana, Dar walisema walipomwona ndugu yao kwenye mitandao walishangaa sana.

Msukule-(2)-001Wakaenda Kituo cha Polisi Mbezi na nguo ili kumvisha lakini walishangaa kuambiwa ndugu yao alitoweka ghafla na hajulikani alipo jambo ambalo wao kama ndugu limewashangaza sana.

Habari hii inaendelea kufuatiliwa, endelea kusoma Magazeti Pendwa ya Global Publishers.

Leave A Reply