The House of Favourite Newspapers

Msuva Afungua Akaunti Ya Mabao Uarabuni

0

KIUNGO Mtanzania, Simon Msuva, ameanza vizuri akiwa na klabu yake mpya ya JS Kabylie huko Algeria kwa kufunga bao katika mchezo wake wa kwanza dhidi ya JSM Bajaia.

Msuva amejiunga na klabu hiyo msimu huu kama mchezaji huru baada ya kuachana na Al-Qadsiah ya nchini Saudi Arabia.

Staa huyo ni kati ya wachezaji walioweka historia ya kufuzu kucheza Kombe la Mataifa Afrika (AFCON) akiwa na kikosi cha Taifa Stars.

Kiungo huyo mwenye kasi, alifunga bao hilo dakika ya 15, katika ushindi wa mabao 5-1 walioupata dhidi ya JSM Bajaia ukiwa ni mchezo wa kirafiki.

Bao hilo alilifunga kiungo huyo katika dakika ya 15, ya mchezo huo ambao wa kwanza kuucheza tangu ajiunge na timu hiyo, katika msimu wake wa kwanza.

Katika mchezo huo, mabao mengine ya JS Kabylie yalifungwa na Faik Amrane, Redouane Berkane na Kouceila Boualia aliyefunga mawili.

Akizungumzia hilo, Msuva alisema: “Nina furaha kubwa kuanza vizuri kwa kufunga bao, ni mwanzo mzuri kwangu, ninaamini nitakuwa nina mwendelezo mzuri mbele.”

STORI NA WILBERT MOLANDI

KISA UMEME KUKATIKA – NAIBU WAZIRI MKUU DOTO BITEKO ATOA TAMKO TANESCO – AMTAJA RAIS SAMIA…


 

Leave A Reply